Mo Simba Awards 2019 ni moto,piga kura yako

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001





Tuzo za Mo Simba zilianzishwa na Mwekezaji katika klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji kwa lengo la kutoa zawadi kwa wanafamilia wa Simba ambao wamesaidia klabu kupata mafanikio kwa msimu wa 2018/2019.

Tuzo hizi zitakuwa na vipengele 12 ambavyo vitahusisha wachezaji na mashabiki.

Kama shabiki wa Simba na soka kwa ujumla unaombwa kupiga kura kuchagua Mchezaji Bora wa Mwaka, Goli Bora la Mwaka, Golikipa Bora wa Mwaka, Beki Bora wa Mwaka, Kiungo Bora wa Mwaka, Mshambuliaji Bora wa Mwaka, Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka na Shabiki Bora wa Mwaka.

Kama kawaida yetu Simba SC vijana wakishafanya kazi ngumu mwisho wa siku tunawapa tuzo. MwanaJF bila kujali unazi biga kura yako kuchagua mchezaji bora katika categories tofauti tofauti. Ingia katika link mosimbaawards.co.tz

Karibu kwa maoni pia
 
Hivi huu uwekezaji wa asilimia 49%kwa asilimia 51% ukoje mbona hatuvioni kwenye soko la hisa Mh Mwakyembe lete ufafanuzi juu ya hili ni suala la wizara yako lakini uko kimyaaa
 
Kura zangu

Mchezaji Bora wa Mwaka-Cloutous Chama

Goli Bora la Mwaka-Chama Vs Nkana

Golikipa Bora wa Mwaka-Manula

Beki Bora wa Mwaka-Nyoni

Kiungo Bora wa Mwaka-Kotei

Mshambuliaji Bora wa Mwaka-Kagere

Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka-Rashid Juma
 
Fafanueni uwekezaji 49% vs 51% hizo zawadi mtapeana tu au mbuzi kauzwa kwenye gunia
 
Kura zangu
Mchezaji Bora wa Mwaka-Cloutous Chama
Goli Bora la Mwaka-Chama Vs Nkana
Golikipa Bora wa Mwaka-Manula
Beki Bora wa Mwaka-Nyoni
Kiungo Bora wa Mwaka-Kotei
Mshambuliaji Bora wa Mwaka-Kagere
Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka-Rashid Juma
Mchezaji bora wa mwaka Emmanuel Okwi. (Imeniuma kwanini hayupo imebidi tu nimuweke) 😭😭
Goli bora la mwaka Chama vs Nkana Red devils
Golikipa bora wa Mwaka Manula.
Beki bora wa mwaka Erasto nyoni.
Kiungo bora wa mwaka Jonas Mkude.
Mshambuliaji bora wa Mwaka John Bocco "Adebayor".
Mchezaji bora mdogo wa Mwaka Rashid Juma.
(Maoni yangu)
 
Ni magoli yapi yanaingia kupigiwa kura.

Iko wapi shortlist kwa kila category!

Au hamna wataalam wa kupembua!!!
 
GOLI BORA LA MWAKA- Chama vs NKANA
MCHEZAJI BORA WA MWAKA- C.C.Chama
GOLIKIPA BORA WA MWAKA- A.Manula
BEKI BORA WA MWAKA- E.Nyoni
KIUNGO BORA WA MWAKA- J.Kotei
MSHAMBULIAJI BORA WA MWAKA- M.Kagere
MCHEZAJI BORA MDOGO WA MWAKA- R.Juma
 
Ni magoli yapi yanaingia kupigiwa kura.
Iko wapi shortlist kwa kila category!
Au hamna wataalam wa kupembua!!!
Magoli yapo manne(4) mkuu.
Chama vs Nkana
Chama vs As Vita
Kagere vs Yanga
Bocco vs Biashara united
 
Goli bora la mwaka --- Mkude vs Nkana

Mchezaji bora wa mwaka--- Kagere

Golikipa bara wa mwaka --- hakuna

Beki bora wa mwaka --- E. Nyoni

Kiungo bora wa mwaka --- C C Chama

Mshambuliaji bora wa mwaka --- Kagere

Mchezaji bora mdogo wa mwaka --- hakuna

Simba Nguvu Moya(in zahera's voice)
 
Ni magoli yapi yanaingia kupigiwa kura.

Iko wapi shortlist kwa kila category!

Au hamna wataalam wa kupembua!!!
Orodha iliyotolewa kwa wanaowania tuzo kwa wachezaji wa Simba ni kama ifuatavyo:-

Wanaowania tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka
James Kotei
Mzamiru Yassin na
Jonas Mkude

Wanaowania tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka
John Bocco
Meddie Kagere na
Emmanuel Okwi

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora
John Bocco
Clatous Chama
Meddie Kagere

Wanaowania tuzo ya golikipa bora

Aishi Manula na Deogratius Munishi

Wanaowania tuzo ya Beki Bora wa Mwaka
Erasto Nyoni
Shomari Kapombe na
Pascal Wawa

Wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo
Paul Bukaba
Adam Salamba na
Rashid Juma

Wanaowania tuzo ya Goli Bora la Mwaka

Clatous Chama VS Nkana FC
Clatous Chama VS AS Vita Club
Meddie Kagere VS Yanga SC
John Bocco VS Biashara United



Zoezi la upigaji wa kura linafanyika kupitia tovuti ya mosimbaawards.co.tz
 
Itaniuma sana sana sana Kama Aishi Manula atapewa tuzo ya Golikipa bora wa Mwaka. Wanasimba wenzangu fusijifariji na huyu Manula, hakuna kitu pale basi tu anallindwa na beki zake lkn pale ni Zerrooo.
Hiyo tuzo irudi kabatini.
Pia mchezaji Chipukizi hao Salamba na Rashid Juma Sifuriiii hawana chochote Tuzo irudi Klabuni hawana jipya kabisa.
Tuzo zingine hizo pa kwa akina Bocco, Kagere, Chama na Nyoni na Kotei.
Mkude hapana kwa msimu huu.
 
Hivi beki bora ameingiaje Kapombe afu shabalala anaachwa
 
Wewe una chuki binafsi na Manula
 
Mikia bwana.. Kapombe trip shamba trip garage.. Anawezaje kumshinda Zimbwe Jr na goli la kusawazisha na As Vita hata sisi tulioko nje mnatoboa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…