Mob psychology inavyoharibu hatima za wengi

Mob psychology inavyoharibu hatima za wengi

MWALIMU DAIMA

Senior Member
Joined
Mar 4, 2023
Posts
129
Reaction score
263
Habari Wana Jf hope wote ni wazima, niende kwenye mada moja kwa moja.
Mob psychology ni Hali jumuishi ya kundi kubwa la watu kuwa na mawazo au mtazamo unao fanana. Kundi kubwa la watu Lina amini kuwa walimu ni watu maskini pia kundi kubwa la watu Lina amini kuwa kusoma hadi chuo kikuu ni kupoteza muda kwani ajira hakuna hiyo ni mifano ya mob psychology.

Mob psychology imeleta madhara makubwa sana kwa maisha ya wa Tanzania Wengi, wasomi na wasio wasomi, mfano Wanachuo Wengi Wana ishi katika msongo wa mawazo kwani akili zao Zina amin baada ya masomo ajira hakuna hii inapelekea afya ya akili kuwa matatani chanzo ni mob psychology.

Katika suala la mahusiano, wanaume wanashidwa kusomesha wachumba zao, sababu Watu wengi wanasema mchumba hasomeshwi hiyo ni athari ya mob psychology.

Vijana wanaogopa kuingia kwenye ndoa kisa tu hawako vizur kiuchumi ( watu wengi husema ili uingie kwenye ndoa lazima uwe vizuri kiuchumi), inapelekea vijana kushidwa kuingia kwenye ndoa chanzo ni mob psychology.

Mob psychology imefanya watu wengi sana kushidwa kufika kwenye hatima za maisha yao,
Mob psychology imeleta umaskini mkubwa kwani watu wamekuwa wa kiiamini kama wengine wanavyo Amini.

Ndugu zangu, ukitazama kama wengine wanavyo tazama basi utakuwa kama wao.
Vijana tuliopo chuo,tusome pasi na msongo wa mawazo kuwa ajira hakuna au maisha mtaani ni magumu, hapana amini ajira zipo na maisha utayamud.

Usitazame kama wengine jifunze kuifikrisha akili yako, kubali kuwa tofauti na mtazamo wa watu hata kama ni Wengi kiasi kipi.

Ni Mimi mwalimu mtarajiwa
 
Sawa mwalimu tunakusubiri kitaa.Mengine yana ukweli ili uingie kwenye ndoa lazma ujipange kiuchumi.
Na tafitti mbali mbali zilishaongesha kuwa the number one cause of marital problems ni lack of money ndani ya nyumba.

Sasa wee ingia kichwa kichwa ukijidanganya kuwa tunapendana. Utakula za uso na matusi ya nguo i ubaki unashanga mwenyewe
 
Back
Top Bottom