'Mobile Banking' inavyozinusuru taasisi za fedha dhidi ya anguko la uchumi

Kande

Senior Member
Joined
Mar 15, 2016
Posts
116
Reaction score
106
Benki ya Equity imezindua huduma ya 'Eazzy Banking' itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kufanya miamala ya fedha popote walipo na wakati wowote.

Akizindua huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Joseph Iha amesema 'Eazzy Banking' inakusudia kusogeza huduma za benki karibu na wateja ambapo wanaweza kufanya miamala yote kwa kutumia simu ya mkononi.

"kila kitu unachofanya kwenye benki sasa utakifanya kwenye App ya Eazzy Banking, kuanzia kutuma pesa, kupata mkopo, kulipia bili au kuangalia mwenendo wa akaunti yako", amesema Iha.

Ameongeza kuwa App hiyo itaokoa muda kwa wafanyabiashara ambao wanatumia kwenda kwenye benki kufanya miamala mbalimbali. "Huu ni usimamizi thabiti, salama na wa uhakika wa fedha na suluhisho ambalo linajumuisha malipo, makusanyo, mapokezi na usimamizi wa fedha kwa ajili ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo", amesema Iha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema huduma hiyo imekuja wakati mwafaka ambapo itawanufaisha wafanyabiashara wa Tanzania ambao wanatumia teknolojia ya simu za mkononi kuratibu shughuli zao popote walipo.

"Ni teknolojia mpya ambayo imeingia Tanzania, itawarahisishia maisha wafanyabiashara, kwanini utumie gharama nyingi kwenda kufuata huduma za benki? nashauri benki ziige ili kupunguza gharama za kufanya biashara Tanzania", amesema Simbeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…