Mobutu Kama Dikiteta, Mobutu Kama Mfano wa Kuigwa

Mobutu Kama Dikiteta, Mobutu Kama Mfano wa Kuigwa

Swadataa

Senior Member
Joined
Dec 9, 2013
Posts
161
Reaction score
65
Mwana JF hutakosea ukisema Mobutu Seseko ni dikteta mbaya kuliko wote kuwahi kutokea katika bara la Afrika. Hata hivyo katika ubaya mkubwa kuna chembe ya uzuri.

Seseko anafaa kuigwa katika msimamo wake wa kuthamini (hata kama alitumika na magharibi) majina ya asili ya kiafrika. Akiwa kijana Seseko aliitwa kwa jina la: Joseph Mobutu. Lakini baadaye akaja kukataza majina ya kizungu kwa wakongomani wote, ikiwemo kufutilia mbali jina lake mwenyewe la ubatizo la Joseph na kujiita; Mobutu Pilipili Sese Seko wa Mabanga (bonge la jina).

Ndio tukubali kuwa waafrika, hasa Watanzania tumekumbatia sana majina ya kizungu, mfano Peter, John, Diana, Catherine n.k wakati tuna majina mengi ya kwetu na wala hamna anayetutishia kutunyonga iwapo tutatumia majina ya kwetu.

Wakati tunalalamika kuwa wazungu walitunyanyasa na wanaendelea kutudharau lakini bado tunajipendekeza kwa kutumia majina yao.

Ingawa naweza kukiri kuwa tabia ya kuwapa watoto majina ya kizungu imeshamiri sana kwa wazazi ambao elimu yao ndogo, ambao naweza kusema hawajaelimika vya kutosha kujua manyanyaso ya wazungu, inasikitisha zaidi msomi anampatia mtoto jina la kizungu. Mbaya zaidi ni pale profesa mzima akiona jina la mwanafunzi wake la Kikurya, Kisukuma au Kinyakyusa anamwambia kompyuta itakataa, jina la kishamba. Kweli?! Tuseme tatizo ni ulimbukeni wa Watanzania kujifanya wanajua Kiingereza, wakati hatujui?

Kuanzia sasa, nadhani tuanze kujitambua tuna majina mengi mazuri.

Kwa kujiita Mobutu Pilipili Sese Seko wa Mabanga na kufutilia mbali jina la ubatizo la Joseph, hadi wakatofautiana na Kadinali wa Kikatoliki (mimi mkatoliki lakini sina jina la Kizungu) na kumrudisha Vatican, dikteta huyu alikuwa sahihi. Tumwige.
 
Hii nayo intelligence???
hivi JF inaelekea wapi?
anyway majina hayasaidii chochote
Tuache porojo tufanye kazi.
 
Kwanza hayo majina ya Mobutu uliyoyaandika siyo yote ys kweli ! Jina lake halikuwa na Pilipili wala Mabanga ! Nenda kasome vizuri au google !
 
Back
Top Bottom