Mofaya imeishia wapi?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Kuna kipindi Diamond aliwapa sana hamasa wasanii wenzake kujikita katika miradi ya biashara pale alipofanikiwa kupiga pesa ndefu alipopewa asilimia kadhaa ya biashara ya "diamond Karanga" yeye akiwa anachangia kulitumia jina lake ili watu wanunue, Diamond akastuka kwamba jina lake ndio chanzo cha mauzo mengi akaona asilimia 30 hazimtoshi, ugomvi ukatokea alipotaka kuongezewa asilimia ziendane na mchango wake ila wale wahindi wakakataa, kilichotokea hadi sasa hizo Karanga zimekuwa historia hazinunuliwi tena maana D hazipi tena promo.

Shilole nae akaona jina analo kwanini asifanye kama Diamond, Shilole akaja na shishi food huduma ya msosi ambayo inafanya poa hadi sasa,

Nae alikiba hakuwa mbali kufuata nyayo za mdogo wake, Jina analo na umarufu anao akaona kwanini aziache pesa ziende bure

Alikiba akaingia makubaliano ya kupewa asilimia kadhaa ya kinywaji cha MOFAYA ya afrika kusini ambayo Alikiba alitaka kuipenyeza Tanzania kwa kutumia umaarufu wake.

Ni muda mrefu hadi sasa promosheni zilifanyika na hata timu ya mpira ya coastal union pia inadhaminiwa na kinywaji hiki, ila cha kushangaza ni kwamba hio bidhaa hadi sasa huenda haijaingia nchini na cha kusikitisha ni kwamba hata amsha amsha ya kukileta hiki kinywaji zimepungua
 
Iliingia I'm proud niliinywa but tena imepotea sijui anakwama wapi.?
 
Wenzio
Wenzio ttunakunywa zimejaa mpaka mikoani.
 

Mofaya inapatikana kwa wingi kwenye videos za Ali Kiba au video za wale vijana wake
 
karanga zinalika Muraaaa....

hiyo mofaya sijawahi iona hata

Chibu zinaendelea budaaah

Shishi yupo sana si unamjua maza ntilie yule anaijua biashara yake
 
Mbona mofaya zipo watu tunakunywa sema ww makani yako uswahili haziuzwi kwa mangi hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…