Mohamed Enterprises yadaiwa kupeleka mbolea feki Songea

Mohamed Enterprises yadaiwa kupeleka mbolea feki Songea

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limeiomba serikali ichukue hatua za sheria kwa kampuni ya Mohamed Enterprises tawi la Songea kwa kile lililochodai kuwauzia wakulima mbolea inayosadikiwa ni feki. Madiwani hao pia wametaka kampuni hiyo iwalipe fidia baadhi ya wakulima kwa kuwasababishia hasara katika msimu wa kilimo wa 2012/13.

Ombi hilo walilitoa katika kikao juzi juzi ambako pia waliwataka meya na mkurugenzi kutoa maelezo yanayojitosheleza kwenye baraza hilo kuhusu hatua zilizokwisha kuchukuliwa kwa kampuni Mohamed Enterprises.

Akizungumza katika kikao hicho, Diwani wa Kata ya Ruhuwiko, Gerad Ndimbo (CCM) alisema anashangazwa mbolea hiyo feki haijateketezwa hadi sasa.

Mbolea hiyo ni sumu hivyo haikutakiwa iendelee kuwapo hadi sasa ikizingatiwa kuwa haijulikani ni kiasi gani kilichomo katika maghala.

Naye Diwani wa Kata ya Bombambili , Keni Mbangala (Chadema) alilitaka baraza hilo kwenda kukagua maghala ya kampuni hiyo kujionea ukweli wa suala hilo kuepusha wananchi kuendelea kutumia mbolea feki.

Diwani wa Kata ya Msamala, Khalifa Mgwasa (CCM) alipendekeza zichukuliwe hatua za sheria ikiwa ni pamoja na kuifungia kampuni hiyo kupeleka mbolea Songea.

Hata hivyo, Meya wa Halmashauri ya Manispaa hiyo, Charles Mhagama alisema halmashauri haina uwezo wa kuibana hiyo kampuni hiyo.

Alisema suala hilo kwa sasa liko ngazi ya mkoa na kinachosubiriwa ni majibu.

Akizungumzia suala hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Joseph Mkirikiti alisema shauri hilo lilikwisha kufanyiwa utafiti wa kina na mwenye kampuni akapewa nafasi ya kujitetea.

DC alisema serikali ilichukua sampuli ya mbolea hiyo kwenda kuifanyia utafiti na kuipima kama inafaa kwa matumizi ya kilimo.

Alipohojiwa, mwakilishi wa kampuni hiyo mkoani Ruvuma, Sadiki Mpemba alipohojiwa na waandishi wa habari alisema hafanyii kazi za majungu za wanasiasa na waandishi.
 
Hao ndiyo majembe ya ccccm hawana uwezo wa kushughulikia jembe lao
 
siku zote daima huwa siamini bidhaa za mohamed hata siku moja na tena huwa sinunui kitu kwake. Vitu vyake vingi anavyouza ni feki
 
Huyu ni mbunge wa Singida Mjini kupitia CCM, mnategemea kuna wa kukemea hilo jambo?
Pesa alizotoa kugharimia uchaguzi zinarudi kwa kuwaadhibu wakulima, bahati mbaya zaidi inawaangukia hata wale ambao hawakuvaa kofia na fulana pia wake zao hawakupenda vilemba na khanga zenye majina ya wagombea hao.
Dewji hawezi kusemwa maana amejenga ofisi za CCM kwenye kata zote za mkoa wa Singida, waanzie wapi pale mjini khanga zina jina lake wanavaa wajinga wanaoshiriki vikao vya maamuzi.
Alistahili kunyongwa au kifungo kirefu, lakini kesho mtasikia anasifiwa kwa kutoa katoni za mafuta ya VIKING
 
hiyo si mara ya kwanza kwani walishatuhumiwa kufanya kitu kama hicho mbeya huyu ndiye aliyekamatwa na chakula kibovu matokeo yake mashaidi wote wakafa na kesi ikafutwa leo anaonekana mtukufu
 
Back
Top Bottom