Mohamed Hussein 'Zimbwe' aheshimiwe

Afisa Tabibu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2021
Posts
511
Reaction score
848
Hivi nikisema huyu ndo namba tatu bora wa muda wote katika ligi kuu ya Tanzania bara nitakuwa nimekosea? Huyu jamaa amecheza kwa kiwango bora kwa misimu karibia kumi mfululizo, amecheza timu ya Taifa mara nyingi mno, ni mchezaji bora sana katika nchi hii.

Nasikitika haheshimiwi, sifa wanapewa wengine yeye anarukwa, tafadhalini sana wanasoka tumpe heshima huyu kijana, sio rahisi kupata mchezaji wa kariba yake kwa miaka hii ya karibuni.
 
Ukitaka ajiuzulu kucheza mpira au ahame namba mwambie amkabe Kisinda au Adebayor
 
Hujakosea....! Kimsingi Kwa Tanzania hasa miaka Ya Karibuni Wachezaji bora wa muda wote karibia namba Zote Wanapatikana Simba tu...!

Nakaribisha povu Kutoka Kwa 'Machale Championi' wa Bongo ..!
 
Hujakosea....! Kimsingi Kwa Tanzania hasa miaka Ya Karibuni Wachezaji bora Wa muda wote karibia namba Zote Wanapatikana Simba tu...!

Nakaribisha povu Kutoka Kwa 'Machale Championi' wa Bongo ..!
Simba hakuna Beki Wa Kati Wa Kitanzania Kama Mwamnyeto Na Job, Hakuna Mido Ya Kitanzania Kama Feitoto Na Kwa Upande Wa Winga Sijaona Simba Winga Wa Kibongo Anayemzidi Chochote Dickson Ambundo....Kama Unabisha Wataje?
 
Simba Hakuna Beki Wa Kati Wa Kitanzania Kama Mwamnyeto Na Job, Hakuna Mido Ya Kitanzania Kama Feitoto Na Kwa Upande Wa Winga Sijaona Simba Winga Wa Kibongo Anayemzidi Chochote Dickson Ambundo....Kama Unabisha Wataje?
Mimi ni Yanga lakini Kuna jamaa wa biashara anacheza namba 7 Renatus Ambrosi na Beki wa Kati wa biashara Abdulmajid Mangalo, hawa jamaa kwasasa wanastahili kuitwa timu ya Taifa.

Huyu Renatus hana mambo mengi yaani angekua Yanga, Mayele angeshafikisha goli 15 mpaka Sasa za ligi kuu.
 
Simba Hakuna Beki Wa Kati Wa Kitanzania Kama Mwamnyeto Na Job, Hakuna Mido Ya Kitanzania Kama Feitoto Na Kwa Upande Wa Winga Sijaona Simba Winga Wa Kibongo Anayemzidi Chochote Dickson Ambundo....Kama Unabisha Wataje?
So Ambundo ni zaidi ya Msuva
 
Abdulmajid Mangalo ......yule jamaa anajitoa sana ....saf
 
Ningekuwa mimi ndiye kocha namuhamishia nafasi ya "Holding midfielder". Ule uwezo wake wa kumiliki mpira jamaa anatisha aisee. Anyway kuna " Zimbwe" mwingine yupo Kibaha hapa though ana miaka minne now.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye mechi zakimataifa kocha ajitahidi kumtafutia wakumzibia anamokosea Mana hua na mapengo yakutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…