Mohamed ' Mo ' Dewji usikubali kutoa Pesa yako kutusajilia Simba SC wachezaji hawa wabovu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Naomba maoni yangu yaheshimiwe kama ambavyo nami pia nitayaheshimu yenu ambayo mtayatoa katika Kuchangia hili ambalo naenda kuligusia hapa kwani naona kuna ' Wapuuzi ' fulani ndani ya Simba SC wanadhani mpira wa miguu walicheza Wao pekee na kwamba wengine hatukucheza na hatuujui.

Nimepokea kwa masikitiko makubwa mno baada ya kusikia Klabu yangu ya Simba imewasajili Wachezaji Adam Salamba na Marcel Kaheza kwa ajili ya kuwatumia katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Kama hii taarifa ni ya kweli basi nakuwa wa Kwanza kabisa kuidharau na kuipuuuza Kamati ya Usajili ya Simba SC na namwomba ' Tajiri ' Mo Dewji asipoteze muda wake kukubali usajili wa hawa Wachezaji wawili.

Ukweli ni kwamba kwa jinsi nilivyowaona hawa Wachezaji wawili Adam Salamba na Marcel Kaheza hawana hadhi ya kuichezea Simba SC labda kama wanasajiliwa kuchezea Kikosi chetu cha Simba B naweza nikaunga mkono usajili wao huu.

Hoja yangu ni fupi tu na ya Kiufundi zaidi….

Adam Salamba
Ni mchezaji ambaye ufanisi wake uwanjani unaonekana katika mechi kama siyo nne au tano ambazo zinahusisha Timu za Simba,Yanga, Azam, Singida na Mtibwa Sugar lakini katika mechi zingine huwa anacheza hovyo sana. Simba SC haiitaji mchezaji wa msimu bali inataka mchezaji wa mechi zote na mwenye tija kwa Timu.

Pia umakini wake awapo uwanjani siyo ule ambao mshambuliaji wa sasa anatakiwa awe nao na kuna mechi kadhaa nimeshuhudia na kugundua kuwa anapenda sana kutumia nguvu nyingi sehemu ambayo hata haiitaji nguvu sana bali inataka tu akili kidogo hali ambayo mara nyingi imekuwa ikimfanya achoke haraka na kupoteza hovyo mipira na pasi zake.

Marcel Kaheza
Ni mchezaji ambaye nikiri kuwa amefanya vyema kwa msimu huu hasa katika Kufunga magoli / mabao ambavyo haikutarajiwa na wengi wetu. Hata hivyo mchezaji huyu ana mapungufu kadhaa ambayo ni kutokujua Kukaba kama akipoteza mipira na pia ana ushambuliaji wa kizamani wa kusubiri atengenezewe ndipo afunge.

Pia Marcel Kaheza ana uvivu na siyo myumbulifu hali ambayo inamfanya basi asiweze kuwa mchezaji tegemeo na mwenye msaada ndani ya Kikosi cha Simba SC ambacho kwa sasa kina jukumu kubwa la kudhihirisha umwamba wake Kimataifa.

MTIZAMO WANGU

Simba SC ya sasa haiitaji ‘ Schoolboys Strikers ‘ kama akina Adam Salamba na Marcel Kaheza bali inahitaji ‘ Clinical Finishers ‘ au ‘ Bull Strikers ‘ ambao wataifanya Simba SC iwe na kati ya 75% hadi 99% ya ushindi kila inapocheza na kwa ‘ uchunguzi ‘ wangu kwa hapa Tanzania kwa sasa bado sijaona aina hii ya Washambuliaji bali nawaona sana wakiwepo Ghana, Zambia na Zimbabwe.

Kama kweli Simba SC inataka kuyaenzi vyema yale maneno ya Mwanasimba mwenzetu Rais wa JMT Dr. Magufuli kwa kufanya vyema basi haina budi kuvunja ‘ Kibubu ‘ na kufanya Usajili kabambe ili tukafanye vizuri huko Kimataifa.

NANI WABAKI NA NANI WAACHWE?

Kama ambavyo huko nyuma niliwahi kusema, kuonya na kupinga usajili wa Kipa Said Nduda na Kuongezewa mkataba kwa Mshambuliaji Laudit Mavugo lakini kwakuwa nilishawaona na kuwasoma kuwa hawana jipya na hawatokuja kuwa na msaada Simba leo tena naendelea kusema kwamba Kipa Nduda na Mshambuliaji Mavugo waachwe kwani hawatufai.

Kwakuwa kunaonekana kuna matatizo kati ya Beki Mganda Juuko Murshid na Uongozi basi nashauri angeachwa tu ili nafasi yake na ile ya Mavugo Simba SC tuitumie katika kuwasajili Washambuliaji wawili tu ‘ mahiri ‘ na ‘ hatari ‘ ambao watakuwa wakisaidiana na akina Emanuel Robert Okwi na John Raphael Boko.

Hata hivyo kama Uongozi wa Simba SC bado una mawasiliano na Mchezaji Mshambuliaji Raia wa Ivory Coast ambaye nilimpenda, nilimkubali na niliumia nilipoona ameachwa aitwae Fredrick Blagnon halafu akaachwa mchezaji mbovu na asiyekuwa na faida Laudit Mavugo basi wafanye nae mazungumzo ili arudi Msimbazi kwani ni aina ya wale Washambuliaji ‘ Bull Strikers ‘ ambao nimewasema.

Mechi zote ambazo niliwahi kumshuhudia Blagnon akicheza Mabeki wa Timu pinzani walikuwa wakikiona cha moto na wengi wao walikuwa wakilala na Viatu vyao baada ya mechi kwani shughuli yake si ya Kitoto.

Nakumbuka kuna siku moja Rafiki yangu wa Siku nyingi na Beki wa Yanga ‘ Mtukutu ‘ Kelvin Yondan a.k.a Cotton aliwahi kuniambia kuwa hakuna Mshambuliaji anayemuogopa kama Fredrick Blagnon kwani ana nguvu sana na hakabiki kiurahisi halafu anajua kucheza rafu za akili ambazo kama ukienda kichwakichwa anaweza akakuumiza vibaya.

Na kama kuna Mshambuliaji ambaye Yondan amekuwa akiniambia kuwa ni mwepesi kukabika basi ni Laudit Mavugo na akasema mara nyingi sana kila akikutana nae katika hizi ‘ derby ‘ zetu za Simba na Yanga Yeye ( Yondan ) huwa anampiga ‘ mkwara ‘ Mavugo mapema tu na Mavugo humuogopa hadi kutoka kabisa mchezoni ila anasema aliwahi kufanya hivyo kwa Blagnon na kilichofuatia alishtukia anapigwa Kiwiko / Kipepsi ambacho kilimuumiza na ikambidi awe mpole na akawa anacheza nae Kiheshima kama siyo Kiutiifu zaidi.

Simba SC hatuna haja ya Kusajili Mabeki kwani tayari tunao wa kutosha na naanza sasa kumtabiria makubwa sana Beki Paul Bukaba kwani anacheza aina ya Beki ile ya ‘ Kazi Kazi ‘ ambayo ilikosekana sana katika Klabu ya Simba na hata Tanzania kwa ujumla. Kutokana na majeraha ya Beki Salim Mbonde nadhani huyu hatotufaa tena hivyo angeachwa tu.

Katika nafasi ya Kiungo sioni haja ya Kuongeza mchezaji yoyote yule kwani kumetosheleza ila nimesikia taarifa kuwa James Kotei anataka kuondoka hivyo niuombe tu Uongozi kumalizina nae mapema kwani ana msaada mkubwa sana katika Kikosi chetu kama ambavyo wote tumeweza kuuona alipocheza karibia katika mechi zake zote alizocheza.

Yangu ni hayo tu GENTAMYCINE.

Nawasilisha.

Cc: Ngushi , MSAGA SUMU , Komeo Lachuma , Gide MK, MACHONDELA
 
Mkuu hebu tuwekee japo statistics zao ili tuone ni kweli hawafai? Ongeza maneno ya kitaalam/kisoka kuwachambua hao wachezaji ili na sisi wengine tuwajue na tupime mzani kama wanafaa au hawafai.
 
Ungekuwa unaelewa mpira ungesema ubovu wao siyo unakuja kubwatuka tu hapa. Elezea kitaalam ubovu wao ni nini... Weka na takwimu hakafu shauri unadhani akina nani wanafaa mbadala wa hawa. Una dada anayejua kucheza mpira? Mlete aje asajiliwe ili roho yako isuuzike
 
Astaghafurulilah!
 
Wabongo Wengi huwa ni wazuri mdomoni!
Mo asipotoa pesa yake utatoa Wewe?
Au Ndio yatakuwa yale ya manji na Yanga.....

Sasa Adam salamba ameshasajiliwa jinyonge [emoji23] [emoji23]
 
Nimewaona hao wachezaji, ni wazuri kuliko Mo Ibrahim na Luizio. Hakuna ubaya wakichukua nafasi zao. Urefu wao ubasaidia kusumbua walinzi. Hawa wakiwa katika timu nzuri ubora wao utajidhihirisha
 
Mkuu hebu tuwekee japo statistics zao ili tuone ni kweli hawafai? Ongeza maneno ya kitaalam/kisoka kuwachambua hao wachezaji ili na sisi wengine tuwajue na tupime mzani kama wanafaa au hawafai.

Nimeshaongeza nyama kama ambavyo umetaka hivyo rudi tena ukasome ' Content ' yangu.
 
Nimewaona hao wachezaji, ni wazuri kuliko Mo Ibrahim na Luizio. Hakuna ubaya wakichukua nafasi zao. Urefu wao ubasaidia kusumbua walinzi. Hawa wakiwa katika timu nzuri ubora wao utajidhihirisha

Sawa.
 
Wabongo Wengi huwa ni wazuri mdomoni!
Mo asipotoa pesa yake utatoa Wewe?
Au Ndio yatakuwa yale ya manji na Yanga.....

Sasa Adam salamba ameshasajiliwa jinyonge [emoji23] [emoji23]

Sawa.
 

Nimeshaongeza nyama katika ' Content ' yangu ya ' Uzi ' hivyo nikuombe tu rudi ukaisome upya ila sikulazimishi ukubaliane na mawazo yangu au mtazamo wangu japo unatakiwa Kuuheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…