Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Diwani wa Kata ya Likombe iliyopo Wilaya ya Mtwara, Mohamed Rashid Musa amefariki dunia leo Alhamisi Septemba 9 saa mbili asubuhi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mtwara, Eliud Shemauya ameiambia Mwananchi kuwa diwani huko amefariki katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula alipofikishwa jana Septemba 8, 2021 baada ya kuugua maradhi ya moyo na kisukari.
Eliud amesema diwani huyo atazikwa kesho Septemba 10, 2021 saa kumi jioni nyumbani kwao mkoani Lindi.
"Kiukweli nyota imezimika, mara ya mwisho alinieleza kuwa ana mpango wa kushirikiana na wananchi wa kata yake kujenga shule ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita, tayari alishamweleza Mkurugenzi wa wilaya yetu mahali ambapo shule hiyo ingejengwa," amesema Shemauya kwa masikitiko.
Kata ya Likombe kwa sasa haina shule ya sekondari.
Kabla ya kuwa diwani, marehemu aliwahi kuwa katibu wa CCM kata ya Likombe kwa kipindi cha miaka kumi.
Chanzo: Mwananchi