Mohamed Said akieleza alivyofikia kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said akieleza alivyofikia kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika

Sawa, nimeipata historia. Lkn kinachoshangaza ni kuwa, kwenye historia unayotaka tuipate, hakuna mchango wa wakristo na wasio dini au wenye dini nyingine wanatajwa.Haiwezekani uhuru uletwe na wazee wa dsm pekee wakati hata vyama vyao vya kazi, makuli n.k vilikuwa na mchanganyiko wa watu wote. Balance mambo, taja wote siyo tu wale wa dini yako.

Kumbuka uhuru haukuwa wa kariakoo, ulikuwa wa Tanganyika yote, kuanzia pwani hadi bara, kanda ya ziwa, kusini mwa tanganyika na kaskazini mashariki na magharibi mwa nchi yetu. Wapo watu walitoa mali zao, walikubali kuachia madaraka yao wote hawatajwi mkuu na wala hatuwajui.

Kwetu BUHA yupo Mwami Ntare, tunaojua mchango wake ni watu walioenda shule kidogo lkn baada ya uhuru alihudumu serikalini kwa muda mchache sana kama naibu waziri wa utamaduni, alipotea mazima tukaletewa kuzika tu mwili wake late 1990s kama sijakosea.

Wapo wengi, kiasi kwamba wote wakitajwa hakuna kitabu cha kuweza kuhimili
 
Back
Top Bottom