Mohamed Said; Mwanahistoria au Mtetezi?

Mohamed Said; Mwanahistoria au Mtetezi?

KAMBOTA

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
176
Reaction score
103
Namwita hapa jamvini ndugu Mohamed Said, nimesoma maandiko kadhaa nikajiridhisha kuwa kitaaluma ni mwanahistoria ila kiuhalisia ni mtetezi wa kundi flani analotaka liwepo kwenye historia, kwa mfano kuhusu Historia ya Tanganyika, hivi kwanini Abdulawaheed Sykes alimwachia Nyerere aongoze chama? hii si dalili kuwa harakati za uhuru zilipata msukumo wa kweli baada ya ujio wa Nyerere?
 
Kitu anachofanya M.Said ni kuonyesha ukweli wa historia iliyofichwa,hata hivyo tunapaswa kujua kwa nini. Mfano Nyerere kuzuia historia ya kweli nani walipigania uhuru w Tanganyika
 
Mohamed said hakika amefanya kazi kubwa sana ambayo ni lazima ithaminike na kinyume chake chuki banafsi koz kaweka ushahidi kibao sasa huo utetezi unatoka wapi?lakini hata ukawa utetezi,ni utetezi wa data kwa hiyo ni sahihi tu
 
Namwita hapa jamvini ndugu Mohamed Said, nimesoma maandiko kadhaa nikajiridhisha kuwa kitaaluma ni mwanahistoria ila kiuhalisia ni mtetezi wa kundi flani analotaka liwepo kwenye historia, kwa mfano kuhusu Historia ya Tanganyika, hivi kwanini Abdulawaheed Sykes alimwachia Nyerere aongoze chama? hii si dalili kuwa harakati za uhuru zilipata msukumo wa kweli baada ya ujio wa Nyerere?

Kambota,
Niwie radhi nimechelewa kuona huu mnakasha na ndiyo maana nimekawia pia
kuchangia.

Umeniita jamvini na nimekaribia.
Kuwa mimi ni mtetezi wa kundi fulani hiyo ni kweli kabisa.

Mimi ni mtetezi wa Waislam.
Kwa nini Abdul Sykes alimwachia Nyerere kiti...

Jibu sitalitoa mimi jibu atalitoa JV Mwapachu, mtoto wa Hamza Mwapachu.
Hebu ingia hapa:

Mohamed Said: FB: JUMA MWAPACHU AMZUNGUMZIA BABA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

Kuwa harakati za uhuru zilipata msukumo mpya kwa kuingia Nyerere katika uongozi wa TAA
na kisha TANU hili ni kweli kabisa.
 
MS mbona uzungumzii uchaguzi unaokuja- UKAWA unawaonaje? mimi naona weye waweza mshauri Lowassa mambo mengi tu pindi aingiapo ikulu
 
Akina Sykes anaowatetea kama wangeshika uongozi wangeharibu sana ni watu wenye majivuno mno.kuna Siku MZEE Kitwana Kondo alitudokeza kuwa hawa akina Sykes ni makapi ya kizulu.
 
Mohamed Said ni Mtetezi wa Waislam. Historia haiandikwi na kila mtu! Wazungu wanasemaga "The winner is the one who write the History" Huo ni ukweli mchungu ambao mimi, wewe na Mohamedi Saidi inabidi tuujue na tuukubali kwakua hakuna namna. Tanzania ina mashujaa kibao achana na hawa wa kiislam ambao Mohamedi Saidi ana waongelea.
 
Back
Top Bottom