Namwita hapa jamvini ndugu Mohamed Said, nimesoma maandiko kadhaa nikajiridhisha kuwa kitaaluma ni mwanahistoria ila kiuhalisia ni mtetezi wa kundi flani analotaka liwepo kwenye historia, kwa mfano kuhusu Historia ya Tanganyika, hivi kwanini Abdulawaheed Sykes alimwachia Nyerere aongoze chama? hii si dalili kuwa harakati za uhuru zilipata msukumo wa kweli baada ya ujio wa Nyerere?
MS mbona uzungumzii uchaguzi unaokuja- UKAWA unawaonaje? mimi naona weye waweza mshauri Lowassa mambo mengi tu pindi aingiapo ikuluKambota,
Niwie radhi nimechelewa kuona huu mnakasha na ndiyo maana nimekawia pia
kuchangia.
Umeniita jamvini na nimekaribia.
Kuwa mimi ni mtetezi wa kundi fulani hiyo ni kweli kabisa.
Mimi ni mtetezi wa Waislam.
Kwa nini Abdul Sykes alimwachia Nyerere kiti...
Jibu sitalitoa mimi jibu atalitoa JV Mwapachu, mtoto wa Hamza Mwapachu.
Hebu ingia hapa:
Mohamed Said: FB: JUMA MWAPACHU AMZUNGUMZIA BABA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
Kuwa harakati za uhuru zilipata msukumo mpya kwa kuingia Nyerere katika uongozi wa TAA
na kisha TANU hili ni kweli kabisa.
MS mbona uzungumzii uchaguzi unaokuja- UKAWA unawaonaje? mimi naona weye waweza mshauri Lowassa mambo mengi tu pindi aingiapo ikulu