Mohamed Salah atwaa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika 2017

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Msukuma ndinga anayewika kupitia Klabu ya Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mchezaji bora kwa mwaka 2017 baada ya kuwabwaga Sadio Mane raia wa Senegal ambaye pia anakipiga Liverpool pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon anayecheza Dortmund ya Nchini Ujerumani.




Timu ya Taifa ya Misri imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka 2017



Asisat Oshoala amenyakua tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka 2017 kwa upande wa Wanawake



Hector Cuper ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa, ametwaa tuzo ya Kocha bora wa Mwaka 2017



Raia wa Zambia, Patson Daka mwenye umri wa miaka 19 ameshinda tuzo ya Mchezaji bora anayechipukia



Huku Klabu ya Wydadi Casablanca kutoka Morocco ikitwaa tuzo ya Klabu bora ya mwaka 2017

 
Namuelewaga sana huyu hanaga makuu yupo serious kweli.
 
Hector Cuper ameshinda tuzo ya kocha bora wa timu ya taifa. Habari imekamilika hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…