Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Bunge ndio sehemu ya wawakilishi wa wananchi, Serikali haiwezi kupokea maoni ya mtu mmoja mmoja kutoka nchi nzima kuhusu suala hili la Bandari.
Kwenye kujadili mkataba, ni wajibu wa Mbunge kupata maoni ya watu wake kwa kuwa ndiye muwakilishi wao, na Bunge hukaribisha maoni kabla ya kupitisha azimio. Mambo haya yote yapo kikatiba, pia yameainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli ya kusema watu hawaafikiani na mkataba huu inategemea na nani anaizungumza lakini Msingi wa Katiba uko wazi.
Mwanasheria Mohamed Salum amesema haya wakati akijibu swali la Mdau lililotaka kujua kwanini Serikali haitaki kusitisha mkataba huu wakati watu wengi wameukataa.
Chanzo: Msemaji Mkuu wa Serikali (Clubhouse)