Mohammed Dewji (Mo), wewe ni msaka noti, achana na akina Salum Abdallah

Mbigirikavu

Senior Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
101
Reaction score
118
Tunajua kuwa wewe Mo ni shabiki na mwanachama wa Simba SC, tunaamini kuna wakati unajitolea kwa hali na mali kuifanya Simba iwe bora sambamba na kuinua furaha yako na mashabiki wenzako.

Lakini kwa sasa tunafahamu kuwa umeingia kwenye mkataba wa kibiashara na Simba SC ambao malengo ni kuongeza ukubwa wa Simba na kuongeza mapato kwa upande wa biashara yako.

Umeikuta Simba ikiwa na uongozi ambao hawakuwa na hela na walizoea hali hiyo, na leo una viongozi hapo Simba wa aina hiyo hiyo. Tofauti sana na wewe uliyezaliwa kwenye hela na umebarikiwa kutambua njia za kuzinasa hizo hela kuliko viongozi wako waliopo hapo.

Kwa hiyo nakukumbusha kuwa kichwa na mhimili wa kuingiza mapato kwenye biashara zako kupitia Simba SC, ni wewe tu Mohammed Dewji.

Usiwaachie timu hao wenye hisa 51% ukatarajia kupata hela hapo Simba. Ingia wewe 'physically'. Hao wengine hawana weledi wa biashara kubwa kama za Mo. Watakufelisha.

Mashabiki wa Simba tunaamini wewe Mo ni chapa kubwa sana Afrika na Duniani kote. Uliypotia mkono wewe panaaminika na wafanyabiashara wengi wakubwa.

Kuna vilabu vikubwa Afrika vinavyomilikiwa na watu uliowazidi mbali sana kifedha, umaarufu, na hadhi. Wewe Mo kuingia kwako kwenye mpira kiuwekezaji kunatazamwa na Afrika nzima kama siyo Dunia.

Hadi kufikia miaka minne ya uwekezaji, kwa tunavyouona utajiri wako Afrika, na ushabiki wako kwa Simba, tulitarajia kuona Simba imebeba Kombe la Mabingwa Afrika.

Wengi tunafahamu kuwa kadiri Simba itakavyokuwa bora ndivyo wadhamini wakubwa watakavyoipigania Simba na mapato ya Simba kuwa makubwa zaidi hatimaye malengo yako ya kuwekeza Simba kibiashara kutimia.

Lakini usithubutu kuwaachia timu watu ambao hawana utalaamu wala utashi wa kweli kuendeleza uwekezaji wako. Watakufelisha na kuangusha chapa yako uliyoijenga barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Ingia wewe, kusajili wachezaji, makocha na vifaa, kama ulivyofanya miaka miwili iliyopita. Akina Salum Abdallah "Try again" wamekuangusha na wataendelea kukuangusha kwa sababu hawajui mifumo ya kibiashara.

Chunguza kidogo tu, timu mwaka juzi, ilitolewa na Kaizer Chief, lakini hiyo Kaizer Chief ndiyo iliyofika fainali. Mwaka jana ilitolewa na Orlando Pirates, nayo ndiyo iliyofika fainali.

Sasa angalia Simba ilivyokuwa dhaifu misimu hiyo. Ingekuwa bora kidogo tu Simba ilikuwa fainali moja kwa moja na leo lingekuwa linaimbwa jina lako kila mahali.

Ubingwa wa Afrika unauchelewesha wewe Mo kwa kuwaachia timu watu wasiyo na malengo ya kibiashara. Wao wanakula, wanalala, wanapata mishara na posho, maisha yanawaendea. Suala la biashara ni la kwako wewe Mo.

Biashara zako zipambanie wewe mwenyewe.

Nakutakia Jumatatu njema.
 
MO ameshafanya upande wake, amesha toa mabilioni ya Bure, ameshatoa mabilioni ya kukopesha timu, ameshatoa mabilioni kama mwekezaji.

Kupitia Mabilioni aliyoyaweka klabu ikaingiza mabilioni pia. Kwasasa kama mfanyabiashara mzoefu, ameshaona hawezi kuingiza mapenzi katika biashara.

Kwasasa amehakikisha miundo mbinu iko sawa na kuiacha klabu ijiendeshe yenyenyewe kibiashara Ili aone Return ya biashara aliyo wekeza na kujipatia faida.

MO hawezi kukaa Simba miaka yote akiwa anatoa fedha tu, kwasasa inatakiwa Simba ijibebe . MO ameacha timu ijiendeshe maana kama fedha alishaweka za kutosha.

Ndio maana Yanga Kila idara Wana ajili watu Kwa professional zao na si kuwa mwanachama mwandamizi.
Yanga upo uwezekano mkubwa wa kupiga hatua Kwa namna wanavyo elekea, kwenye mambo mapya wanatafuta professional ata kutoka nje Ili wawasaidie katika eneo walilo kusudia.
 
Kupitia Mabilioni aliyoyaweka klabu ikaingiza mabilioni pia.
Kwasasa kama mfanyabiashara mzoefu, ameshaona hawezi kuingiza mapenzi katika biashara.

Kwasasa amehakikisha miundo mbinu iko sawa na kuiacha klabu ijiendeshe yenyenyewe kibiashara Ili aone Return ya biashara aliyo wekeza na kujipatia faida.

MO hawezi kukaa Simba miaka yote akiwa anatoa fedha tu, kwasasa inatakiwa Simba ijibebe . MO ameacha timu ijiendeshe maana kama fedha alishaweka za kutosha.
Ndio maana Yanga Kila idara Wana ajili watu Kwa professional zao na si kuwa mwanachama mwandamizi.
Yanga upo uwezekano mkubwa wa kupiga hatua Kwa namna wanavyo elekea, kwenye mambo mapya wanatafuta professional ata kutoka nje Ili wawasaidie katika eneo walilo kusudia.
1. Mo ni rais wa simba. Mafanikio.ya simba ni yeye na kufeli kwa simba ni yeye. Hawezi kukwepa

2. Mo ameweka mpunga wake kwa kibiashara. Kupata faida ni yeye na kupata hasara ni yeye. Hawezi kukwepa
3. Mo hajajiondoa simba, ila ameweka watu kwenye nafasi yake. Wakianguka, amenguka mo, na wakisimama, amesimama mo.
 
MO ameshafanya upande wake, amesha toa mabilioni ya Bure, ameshatoa mabilioni ya kukopesha timu, ameshatoa mabilioni kama mwekezaji.

Kupitia Mabilioni aliyoyaweka klabu ikaingiza mabilioni pia. Kwasasa kama mfanyabiashara mzoefu, ameshaona hawezi kuingiza mapenzi katika biashara.

Kwasasa amehakikisha miundo mbinu iko sawa na kuiacha klabu ijiendeshe yenyenyewe kibiashara Ili aone Return ya biashara aliyo wekeza na kujipatia faida.

MO hawezi kukaa Simba miaka yote akiwa anatoa fedha tu, kwasasa inatakiwa Simba ijibebe . MO ameacha timu ijiendeshe maana kama fedha alishaweka za kutosha.

Ndio maana Yanga Kila idara Wana ajili watu Kwa professional zao na si kuwa mwanachama mwandamizi.
Yanga upo uwezekano mkubwa wa kupiga hatua Kwa namna wanavyo elekea, kwenye mambo mapya wanatafuta professional ata kutoka nje Ili wawasaidie katika eneo walilo kusudia.
Umeandika kitu muhimu sana ukiachana n uredio mbao wako
 
Manara na mzee mpili wana professional gani
 
Mo Alijitoa wakati wa Usajili.

Mimi ni Simba Damu lakini Mo nae mda mwingine CHUPLI sana.

Tuna wachezaji wakawaida na wabovu mno

Dejan.
Okwa.
Akpan.
Onyanga.
Sackho.
Banda.

.........................................
Boko.
Nyoni.
KIBU.
Kapama.
Kyombo.
Mwenda.
Gadiel nk....
 
Anatakiwa afikirie zaidi brand yake. Sisi mashabiki ni kufahisha mioyo yetu tu. Yeye atafurahi kama shabiki na atafurahia kukuza biashara zake na brand yake pia.
 
Mo Alijitoa wakati wa Usajili.

Mimi ni Simba Damu lakini Mo nae mda mwingine CHUPLI sana.

Tuna wachezaji wakawaida na wabovu mno

Dejan.
Okwa.
Akpan.
Onyanga.
Sackho.
Banda.

.........................................
Boko.
Nyoni.
KIBU.
Kapama.
Kyombo.
Mwenda.
Gadiel nk....
Yawezekana ni wachezaji wazuri ila kuna vitu wanavikosa.
Sasa hivi viongozi wanawaza kutafuta kocha wa viungo. Wachezaji waliozoea kuwa na kocha bora wa viungo, wamecheza kwa zaidi ya miezi miwili bila kocha bora wa viungo.
Tutafakari hapo.
 
Mo Alijitoa wakati wa Usajili.

Mimi ni Simba Damu lakini Mo nae mda mwingine CHUPLI sana.

Tuna wachezaji wakawaida na wabovu mno

Dejan.
Okwa.
Akpan.
Onyanga.
Sackho.
Banda.

.........................................
Boko.
Nyoni.
KIBU.
Kapama.
Kyombo.
Mwenda.
Gadiel nk....
Kama ni wa kawaida mbona wapo makundi Africa ,au unahisi wamebahatisha?

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mo Alijitoa wakati wa Usajili.

Mimi ni Simba Damu lakini Mo nae mda mwingine CHUPLI sana.

Tuna wachezaji wakawaida na wabovu mno

Dejan.
Okwa.
Akpan.
Onyanga.
Sackho.
Banda.

.........................................
Boko.
Nyoni.
KIBU.
Kapama.
Kyombo.
Mwenda.
Gadiel nk....
Kassim dewji alimshauri babra team iwe na technical director Ila babra akakataa.

Sasa hayo ndio matokeo.

Hapo Ni hauwezi kumlaumu kwasababu yeye anatoa hela tu wala hafanyi any recruitment process.
 
Back
Top Bottom