Mohammed Hosny,mtaalamu wa lugha ya kiswahili kutoka Misri,

Mohammed Hosny,mtaalamu wa lugha ya kiswahili kutoka Misri,

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775




Lugha ya Kiswahili ni lugha maarufu sana katika ukanda wa Afrika ya mashariki hasa nchini Tanzania ambako asilimi kubwa ya watu wake wanakizungumza Kiswahili katika maelewano mazuri licha ya changamoto za kilafudhi zilizopo katika sehemu mbalimbali ambazo bado pia hazina athari kubwa katika kuporomosha lugha ya Kiswahili.


Si jambo la ajabu leo hii kukutana na watu wengi watokao mbali na nchi za ukanda wa Afrika mashariki wkijifunza na kuzungumza sana lugha hii kama vile na wao ni wazaliwa wan chi za Kiswahili.

Hali hiyo inatia hamasa kubwa sana kwa vijana wengi wazungumzaji na wasio wazungumzaji na wao kujifunza ama kujiendeleza katika lugha ya Kiswahili.

Mwaka jana niliandika mahojiano mafupi nilofanya na mtaalamu wa Kiswahili kutoka nchini Misri ambae alikuwa mwanafunzi na baadae kuwa mwalimu wa lugha ya Kiswahili.
Mohammedi Yousri Mswahili likiwa ndio jina lake maarufu.

Lakini leo tena tarehe moja ya mwezi wa kwanza mwaka 2018,nakuletea makala nyingine ya mtaalamu wa Kiswahili kutokea huko huko nchini Misri,Mohamed Hosny.
Najua ni wengi sana kati yetu watakuwa hawafahamu kuwa Kiswahili ni moja kati ya lugha za kitafiti katika nchi ya Misri na wazungumzaji wengi wakiwa ni wasomi waliobonbea katika masuala ya lugha za kiafrika katika chuo kikuu cha Misri.

Mohammed Hosny alizaliwa tarehe 29 ya mwezi wa kumi Mwaka 1989 katika nchi ya Misri.
Alizaliwa katika eneo la Al Khanka mkoa wa Al Khalyubiya Misri ila kwa sasa Hosny anaishi katika mji mkuu wa Cairo.
Pia Mohammed Hosny alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Al Azhar,moja ya vyuo vikuu maarufu duniani vilobeba katika ufundisha wa masuala mbalimbali yakiwemo yale ya lugha za kimataifa.





















Mohamed Hosn anasema,walimu wake wengi wa lugha ya Kiswahili ni raia ya Misri na pia NI raia wa Tanzania na hata alipokuja Tanzania likutana na baadhi ya walimu wa Kiswahili ambao walimfundisha na hata marafiki wake wale wa asili ya kimasai walimfundisha kuzungumza baadhi ya maneno katika lugha ya kimaasai.









Mohamed Hosny,kulia
Anasema aliipenda sana Tanzania hata kupenda baadhi ya timu za mpira wa miguu huku timu ambayo anaipenda zaidi ni ile ya Yanga na huku timu ya Misri aipendayo ni Zameleki ambayo mara kadha tumeshuhudia ikifanya mashindano na timu za Tanzania kama Simba ya Dar es salaam
Anamkubali sana mchezaji Mbwana Samata ambae alijizolea umaarufu mkubwa katika bara la Afrika baada ya kupewa tuzo ya mchezaji bora.

Mohammed Hosny ni muhitimu katika chuo kikuu cha AL Azhari kitivo cha lughana ufasiri kitengo cha lugha za kiafrika akiwa amehitimu mwaka 2014.


Makala hii imeandikwa na mimi Idd Ninga
Simu namba +255624010160

iddyallyninga@gmail.com

nitaendelea kuwaletea taarifa mbalimbali zihusuzo Kiswahili panapo uhai na maajaliwa yake mwenyezi.

at December 31, 2017
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
No comments:
 
Back
Top Bottom