Mohammed hussein (Zimbwe jr): Sindano ilishona koti la suti

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Ni Katikati ya mwaka 2013, zimbwe jr yupo kwenye basi la kagera Sugar anamtoroka meneja wake Heri Mzozo ili akasaini mwaka mmoja na wanankurukumbi. Hii ni baada ya tindikali za moto zilipounguza moyo wake akiwa Azam academy ambapo vijana aliyocheza nao hapo (simon Msuva na Aishi manula) walishaanza kutoboa. Huku kocha Stewart Hall akimuondoa Zimbwe na wenzake Kambini.
.
Zimbwe anaona maisha ni kama mlima uliyomlalia kifuani. Lichw ya akili za kitoto za Zimbwe, Heri Mzozo akafanya juu chini na mungu si Athumani zimbwe akasaini simba, enzi hizo yupo Isa Rashid baba Ubaya na Abdi Banda. Mbavu zilizo shiba, Zimbwe jr anajiuliza je "nitatoboa kweli?" Mungu anaonesha miujiza yake, Abdi banda anabadilishwa namba huku Baba ubaya yupo Majeruhi. Ni zimbwe pekee aliyebaki kuzilinda mbavu za mnyama. Anapewa nafasi kisha anafanya maajabu.
.
Naam hiki ni kisha kifupi cha Zimbwe na Simba. Leo naongea nanyi watanzania kisha nitaongea na Zimbwe.
Samuel Goldfish ni Producer mkongwe wa filamu Marekani, yeye aliwahi kusema "“The harder I work, the luckier I get.” kadri anavyofanya kazi ndivyo kadri anavyopata bahati. Nataka kuwaambia si Uchawi wala fitna, bali ni juhudi ndiyo zinamfanya zimbwe awe maridadi kazini.
.
Tanzania ina mbavu imara za kushoto, kama kisiki basi ni cha Mpingo, na kama laini basi ni kama muwa bungala, zimbwe yupo kama spana malaya, kila mfumo yeye twende tu, ukitaka Pira gumu yuko tayari, ukitaka pira Laini (biriani) twende. Si uchawi, ni juhudi tu.
.
Sasa naongea na wewe zimbwe, "Alipangalo Mola Huwa" yuko wapi tena Yupo wapi Tena Jamal Mwambeleko, nioneshe alipo Asante kwasi, amekwenda wapi Stephano mwasika? Basi jua kwamba huu ni wakati wako, mungu amekufungulia milango ya riziki, ingia jibwede mwanaume, wahenga walistaajabu sana kuona wembamba wa Reli lakini Treni Ilipita juu yake, leo Afrika inashangaa umbo lako na mambo yako, waache washangae tu, kama majibu hawana basi wakaliangalie koti la suti, ni kubwa mno, lakini lote linashonwa na kasindano kadogodogo.
.
Asante kwa burudani yako ewe Digi digi mwenye mapafu ya farasi wa vita. The time is yours, use it.
official_mohamedhussein15-___CNFw5Mbrs4n___-.jpg
official_mohamedhussein15-___CMfP5nRLHlz___-.jpg
official_mohamedhussein15-___CNNbEcwr2yb___-3.jpg
 
View attachment 1742985View attachment 1742986View attachment 1742987
Wahenga walishasema ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi
 
Asante kwa story fupi ya el CAPTAIN

Ila kiukweli Zimbwe Jr ni moto kweli kweli, ameimarika sana sana,,, huwa nafarijika sana nikimuona uwanjani siku hiyo hasa katika hizi mechi za klabu bingwa

Kwanza, anajua kufanya tackling, ana Ball control inayomuwezesha kucheza Biriani style yaani mletee mpira wowote ule uwe wa juu, chini, kimo cha kuku au mpira wa ugoko atautuliza kama vanny Boy alivyomtuliza Paula, ana speed nzuri anapokwenda kushambulia, na anajua kuyamwaga maji au kupiga ndizi ili kina Mugalu wajimwaye mwaye

Japo ana udhaifu mmoja tu, anapopanda kwenda kushambulia anakuwa slow ktk kurudi kuja kucover space aliyoiacha

Ila all in all, ni moja ya mabeki bora kabisa nchini kwa sasa kwenye mbavu ya kushoto
 
Ni mzuri ila anaweza kuwa mzuri zaidi kama atarekebisha mapungufu kadhaa kosa lake la kwanza ni kujiposition anapenda kuingia ndani zaidi upande wa beki zq kqti badala ya kukaa nafasi yake, akikutana nq winga mwenye speed ni tatizo kwake, pasi zake nyingi ni za uchonganishi pia anapenda kukaa sana na mpira badala ya kutoa pasi kwa haraka
 
Kwao ni kigoma ujiji na alikuwa ni mchezaji wa wizard Fc ya kigoma na baadae Saigoni fc na Fc bandari zote za kigoma
Zimbwe Junior Mo hussein Tshabalalah noma sana huyu jamaa
Iv ni mtu wa wap huyu jamaa ??
By the way big up sana kwake
 
Back
Top Bottom