Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesema hatogombea nafasi ya ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwakuwa bado ana kazi ya kukitumikia Chama cha Mapinduzi na Vijana wa Tanzania.
Kawaida amesema hayo jana Aprili 14, 2025 mkoani Njombe katika mahojiano na kituo cha radio cha Kings FM kwenye kipindi cha Kingdom kinachoendeshwa na Mfaume Pastory na Deo Mgina.
Kawaida yupo mkoani Njombe katika ziara ya kikazi na kuhamasisha vijana kujitokeza kugombea nafasi ya Ubunge na Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi kwakuwa yupo tayari kuwapambania ili kupata nafasi hizo.