Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Cde. Mohammed Ali Kawaida (MCC) ameomba Chama cha Mapinduzi (CCM) kiwakabidhi vijana hao kushughulika na chama cha upinzani Zanzibar (ACT - Wazalendo) ambao wamekuwa wakikejeli maendeleo makubwa ambayo yanafanyika katika Visiwa vya Zanzibar pia kukashifu viongozi na Mapinduzi Matukufu na kusema UVCCM itahakikisha inapambana nao katika mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu 2025.