MOI: Upasuaji wa kunyoosha mfupa wa mgongo uliopinda wafanyika

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa kunyoosha mfupa wa mgongo wa mtoto uliopinda (kibiongo) kitaalam unafahamika kama ‘Scoliosis’.

Upasuaji huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini ulitumia teknolojia ijulikanayo kama 'Posterior Instrumentation and Fusion' ambayo inahusisha uwekaji wa vyuma maalum kwenye mfupa wa mgongo katika sehemu ya juu na chini ya mfupa wa mgongo na kuufanya mgongo unyooke.

Akizungumza leo Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dk Othman Kiloloma, alisema uanzishwaji wa upasuaji huo umetokana na kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimafunzo kati ya taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha madaktari bingwa wa upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini COSECSA na madaktari bingwa kutoka Marekani.

Source: MOI yafanya upasuaji wa kunyoosha mfupa wa mgongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…