Moja kati ya nukuu bora kabisa kutoka kwa Hayati Magufuli

Moja kati ya nukuu bora kabisa kutoka kwa Hayati Magufuli

Pendaelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
11,050
Reaction score
31,412
Tukiacha mambo kiasa Magufuli alikua muhamasishaji mzuri sana.

Kipande hiki cha hotuba yake hii nimetumia kama falsafa ya maisha yangu.
Ni bora kufanya ukosee kuliko kuto kufanya, ni wazi kwenye makosa ndiko kuliko na faida nyingi kuliko kupatia, vitu vingi tunavyo viona vimetokana na makosa, waliofanya wakakosea kama wasingefanya kwa kuogopa kukosea dunia isingekua ilivyo sasa.

Pia kufanya maamuzi kumechangia vitu vingi kusimama, mtu unapokuwa na maamuzi ya kusita sita na kuahirisha mipango yako mara nyingi hujikuta ukihesabu miaka tu bila kupiga hatua, usipo amua huwezi kufanya chochote.

Aendelee kupumzika kwa amani, aliacha athari nyingi sana kwetu kama taifa hata mtu mmoja mmoja, kama utamsikiliza kwa sikio la nje ya siasa.
 
Back
Top Bottom