Maisha ya soka hapa Tanzania yamejaa maswali mengi sana.Unaweza ukafikiri mpira ni kipaji,uwezo,nidhamu na kujituma sana katika mazoezi.Kwa hapa Tanzania jibu ni lah!
Watanzania wengi wakiwemo viongozi wa timu hizi wanaamini kuwa mchezaji anaweza kurogwa kupitia mahusiano ya kimapenzi na mwanamke kiasi kwamba anaweza kuathiriwa uwezo wake wa kuonyesha kipaji chake.
Imani kama hizo ambazo sio za kiweledi kabisa,zinasababisha timu yenye wachezaji wakubwa kuwekwa kuishi kambini na kuziacha familia zao nyumbani.
Hivi mtu ana mke na watoto,anawezaje kuishi Avic town mke anamwacha Tegeta?
Huyo mke mnamsaidiaje kihisia au mnadhani pesa inaaweza kumaliza changamoto zote?
Wachezaji wanatakiwa kuwekewa utaratibu wa kuwadhibiti kwenye nidhamu nje ya uwanja pasipo kuwapoka uhuru wao.Huwezi kuishi mwaka mzima kama mwanafunzi wa sekondari boarding wakati wewe ni professional player.
Tuache fikra za kichawi tunapoendesha soka la kisasa,wachezaji washindane kwa vipaji na uwezo wao uwanjani na sio mazingira ya nje ya uwanja kama inavyofanyika kwetu
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app