Moja ya hoja Maalim Seif kwa SUK ni Masheikh wa Uamsho kuachiwa au kesi yao isikilizwe

Moja ya hoja Maalim Seif kwa SUK ni Masheikh wa Uamsho kuachiwa au kesi yao isikilizwe

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Rais wa Zanzibar yupo na Mtizamo tofauti kuhusu Zanzibar, pamoja na kwamba anajua aliingia kwa njia zenye vitendo vya kidemokrasia bado anatambua kwamba bila Zanzibar moja hakuna maendeleo.

Amejaribu alivyoweza kumvuta Maalim Seif karibu kwa lengo lakupunguza machungu lakini bado hajaondoa kilio Cha wengi.

Rais wa Zanzibar anayo nafasi ya kuangalia upya namna yakujadili na Maalim seif kuona viongoz wa Uhamsho wanaachiwa au kesi yao kusikilizwa kisha wahukumiwe wajue wanatumikia kifungo.

Lakini pia lipo Jambo kubwa la kimuungano ambalo limeibuka baada ya baraza la Mawaziri kutangazwa, nadhani ipo shida hasa pale Mawazir wote wanapotoka Znz na pale Manaibu wanapoonekana wawili tu kwenye baraza.

Jambo la mwisho nikutengeneza maridhiano baina ya wazanzibar na si maridhiano yakisiasa kwa manufaa ya viongozi.
 
Mheshimiwa sana Raisi Hussein Ali Hassan Mwinyi akitaka kupotea kisiasa 'yeye kama yeye ama CCM Zanzibar' basi aombe/au ashawishi kuachiwa kwa hao mashehe wa taasisi ya JUMUKI (maarufu kwa jina la mashehe wa uamsho)

Kuachiwa kwa hao mashehe ambao pia walikuwa wakijihusisha na siasa kunaweza kuwapatia zaidi umaarufu, ambao pia unaweza kumfunika yeye na CCM Zanzibar
 
Sio kweli. Hao masheikh hawana ushawishi wowote wa kisiasa, ushawishi wa kisiasa zanzibar ni matokeo ya umaskini unaokua siku hata siku huko visiwani. Mwinyi akiweza kujenga uchumi utakaoleta fursa za ajira na kurudisha "currency flows" kati ya zanzibar na UK, Oman atakuwa amefanya jambo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom