Moja ya kesi zilizokuwa ngumu, gumzo na ya kihistoria duniani, O.J Simpson akihusika

Kiongozi, kesi hii si tu ilikuwa maarufu ila ilishawishi sana watu kufikiri vyema kuhusu the Jury na Mamlaka yake. Mbali na hilo Kuna baadhi ya mambo yamenifikirisha na kunivutia kwenye post yako:

1. Kesi hii ilihusisha Mapambano makali kuhusu ushahidi baina ya Mawakili wa Jamuhuri na mawakili wa mteja (mawakili binafsi). Uchambuzi wako kwa namna ya pekee haukujikita kwenye kambi yeyote. Kwa maneno mepesi umetimiza wajibu wako kama muandishi. Asante sana.

2. Lipo jukwaa la Sheria. Hukuona vyema kutoa hii habari huko (sina uhakika). Kutoka moyoni kama ndivyo ilivyo, nakuunga mkono hasa kwa hoja kwamba jukwaa husika limeachwa kwa wauliza maswali na si watoa mihadhara na wachangiaji. Ni kama bado Jukwaa husika halija fahamu kwamba kwenye professional duties haitoshi tu kuuliza maswali.

3. Sheria, kama ulivyo jaribu kuitanabaisha kwenye Article yako ni moja ya professions za au zinazotumika kiinteligensia (inteligensia hapa itambulike kwa tafsiri yangu kwamba ni uwezo wa kipekee wa kufikiri. Nothing more nothing less). Taaluma hii inajikita kwenye maajabu ya kugundua haki, "haki", msamiati mpana lakini tunaolazimika kuutafsiri kila siku.

4. Kuna hoja za mwisho ulizo eleza kwenye makala yako (kama ulikusudia kuwa ni makala). Hoja hizi zimetibu Mashaka ya msomaji yeyote. Mashaka kwamba: je mtu anaweza ku commit perfect murder?. Maelezo yako ya mwisho yana umuhimu sana kwa Jamii. Kwa waliokuelewa vyema wameweka hili wazi, kwenye post zao: wameeleza: kwa maneno rahisi yasiyo ya kitaaluma kwamba "damu ya marehemu inamfuata OJ!".

5. Tafadhali niruhusu kwenye namba hii (5). Nieleze machache tofauti kiasi fulani na theme ya post yako:

i. Nafikiri unaupeo mkubwa wa kufikiri. Napata shida na jina lako hapa, hatahivyo kwa namna ya pekee nashawishika kwamba ulimaanisha kitu, kitu ambacho labda kinasadifu mrengo wa fikra zako.

ii. Ipo jumuiya kubwa ya waandishi ambao kwa uandishi wako angalau unawapa moyo. Uandishi wa kisasa, uandishi ambao hautungi jambo jipya, uandishi unaojikita kwenye mambo yaliyojiri. Huu ni uandishi wa pekee kiongozi. Uandishi unaovutia kwa sasa. Fiction zimepoteza mvuto kwenye kizazi hiki (labda, ila ni fikra zangu tu).

Mwenyezi Mungu akupe nguvu Kiongozi. Namuona mtu anaenivutia nami kusema baadaye. Asante sana your excellence!!.
 
Naikumbuka sana hii kesi ya O.J Simpson miaka ile ya 90.
Ahsante kwa uzi mzuri.
 
Ukiangalia series kama how to get away with murder unagundua waliopo jela sio wenye hatia.
 
Hii story ya O.J ndio imechezwa kwenye series ya American criminal story.Kiongozi chizi maarifa umeelezea vema sana hongera Jury ni balaza la waamuzi.
 
Niliangalia Investigation Discovery siku moja wanaamini O.J Simpson sio muuaji bali mdogo wake O.J ndo alitumika kufanya hilo tukio,hii kesi ni shiida inasikitisha sana.. Ss sijui ukweli ni upi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…