Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Nimefanya kazi kwenye Microfinance kwa miaka kadhaa ya nyuma na moja ya kosa kubwa nimekua nikiliona kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wasio wafanya biashara wengi ni uelewa mdogo juu ya maswala ya Financial au mikopo kwa ujumla mwisho wa siku biashara ina kutwa na mawili kati ya haya.
Kwa wale watumishi wa serikali, anakopa apeleke mtoto shule yaani ADA mtoto akienda shule anaanza kulipa mkopo kwa RIBA kubwa. Huku chakula hana Mshahara Laki 240,000 /= hapo hapo alipe Mkopo humo humo Avae, Auguze, Anunue Dawa, Chakula na mtoto kule Shuleni anataka mahitaji madogo madogo huku akiangalia Mkopo haujasogea matokeo yake anakuwa tapeli wa Makampuni mengine likiwamo na lile lililomuwezesha kupeleka mtoto shule.
Kitakachofuata hataingia kazini, kama ni mwalimu atakuwa na kipindi kimoja tena cha mapema vingine vyote hafundishi ukichanganya na stress, mawazo bado wanaomdai wanamfuatilia kazini kwake mwisho wa siku anaanza utolo kazini na kuingia kipindi chake mara moja moja watoto hawa somi kwa wakati. Mwisho wa siku watamfukuza kazi chanzo kikuu ni kwa sababu ya madeni.
1. Biashara haikui hivyo anazunguka palepale miaka nenda miaka rudi.
Kosa kubwa wafanyabiashara wamekua wakifanya unakuta mtu anakopa ili aaanzishe biashara mpya hivyo anakua na stress mara mbili za kulipa mkopo huku wakati huo huo akianza kukuza biashara mwisho wa siku kimoja kinafeli na mnavyojua stress za madeni weeee acha kabisa.
Kosa jingine mkopo wako unaupeleka kwenye biashara ambayo huna mzunguko mzuri, wateja huna na mazingira ya biashara sio rafiki katika mzunguko wa mfanyabiashara mtaji wako ni mdogo kulinganisha na mkopo uliochukua ukija kujulisha na kodi, tozo za bidhaa huo mkopo utautazungusha wiki umeisha na hela huioni imekwenda wapi.
2. By the time kamaliza marejesho na biashara ndo imekufa.
Kosa lingine unakuta Kampuni imempa RIBA ya asimilia 18+% alafu yeye faida yake ni asilimia 10% tu mwisho wa siku ana hasara ya asilimia 8…. Unadhani kwa nini asirudi kukopa tena!
Wengine wanakopa bila utafiti mwisho wanakua watumwa wa madeni, sasa mtu atakua akiniuliza sasa nizingatie nini ninapokopa
ZINGATIA MOJA YA HAYA MAMBO KADHAA KABLA YA KUKOPA
1. Fanya Tafiti ya Biashara yako na uone kweli kama unahitaji kukopa,
2. Kopa ili kukuza Biashara ambayo umeisha ielewa mahesabu. Nje na hapo aisee utatuletea ushuhuda,
3. Kuwa makini na kitu gani unaweka bondi nimeona Nyumba za watu zikiuzwa Familia ikibaki kuteseka.
Kabla sijaendelea naomba unifollow ili kuendelea kujifunza na sitakuwa mchoyo wa maarifa.
Ukikopa kwa ajili ya biashara hakikisha pesa zinaenda kwenye biashara na sio matumizi nje ya business. Nimeona wengi wakitumia mkopo nje ya sababu walizokopea na kwenye biashara ukipunguza hata mia ujue umeinyonga biashara yako… Nitaendelea wakati mwingine
Kama umejifunza basi like share ili na wengine wajifunze pia maswala ya Fedha na mikopo ya benki.