Moja ya mambo ambayo watu hufanya makosa ni kwenye kuchukua mikopo!

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Nimefanya kazi kwenye Microfinance kwa miaka kadhaa ya nyuma na moja ya kosa kubwa nimekua nikiliona kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wasio wafanya biashara wengi ni uelewa mdogo juu ya maswala ya Financial au mikopo kwa ujumla mwisho wa siku biashara ina kutwa na mawili kati ya haya.

Kwa wale watumishi wa serikali, anakopa apeleke mtoto shule yaani ADA mtoto akienda shule anaanza kulipa mkopo kwa RIBA kubwa. Huku chakula hana Mshahara Laki 240,000 /= hapo hapo alipe Mkopo humo humo Avae, Auguze, Anunue Dawa, Chakula na mtoto kule Shuleni anataka mahitaji madogo madogo huku akiangalia Mkopo haujasogea matokeo yake anakuwa tapeli wa Makampuni mengine likiwamo na lile lililomuwezesha kupeleka mtoto shule.

Kitakachofuata hataingia kazini, kama ni mwalimu atakuwa na kipindi kimoja tena cha mapema vingine vyote hafundishi ukichanganya na stress, mawazo bado wanaomdai wanamfuatilia kazini kwake mwisho wa siku anaanza utolo kazini na kuingia kipindi chake mara moja moja watoto hawa somi kwa wakati. Mwisho wa siku watamfukuza kazi chanzo kikuu ni kwa sababu ya madeni.

1. Biashara haikui hivyo anazunguka palepale miaka nenda miaka rudi.

Kosa kubwa wafanyabiashara wamekua wakifanya unakuta mtu anakopa ili aaanzishe biashara mpya hivyo anakua na stress mara mbili za kulipa mkopo huku wakati huo huo akianza kukuza biashara mwisho wa siku kimoja kinafeli na mnavyojua stress za madeni weeee acha kabisa.

Kosa jingine mkopo wako unaupeleka kwenye biashara ambayo huna mzunguko mzuri, wateja huna na mazingira ya biashara sio rafiki katika mzunguko wa mfanyabiashara mtaji wako ni mdogo kulinganisha na mkopo uliochukua ukija kujulisha na kodi, tozo za bidhaa huo mkopo utautazungusha wiki umeisha na hela huioni imekwenda wapi.

2. By the time kamaliza marejesho na biashara ndo imekufa.

Kosa lingine unakuta Kampuni imempa RIBA ya asimilia 18+% alafu yeye faida yake ni asilimia 10% tu mwisho wa siku ana hasara ya asilimia 8…. Unadhani kwa nini asirudi kukopa tena!

Wengine wanakopa bila utafiti mwisho wanakua watumwa wa madeni, sasa mtu atakua akiniuliza sasa nizingatie nini ninapokopa

ZINGATIA MOJA YA HAYA MAMBO KADHAA KABLA YA KUKOPA

1.
Fanya Tafiti ya Biashara yako na uone kweli kama unahitaji kukopa,

2. Kopa ili kukuza Biashara ambayo umeisha ielewa mahesabu. Nje na hapo aisee utatuletea ushuhuda,

3. Kuwa makini na kitu gani unaweka bondi nimeona Nyumba za watu zikiuzwa Familia ikibaki kuteseka.

Kabla sijaendelea naomba unifollow ili kuendelea kujifunza na sitakuwa mchoyo wa maarifa.

Ukikopa kwa ajili ya biashara hakikisha pesa zinaenda kwenye biashara na sio matumizi nje ya business. Nimeona wengi wakitumia mkopo nje ya sababu walizokopea na kwenye biashara ukipunguza hata mia ujue umeinyonga biashara yako… Nitaendelea wakati mwingine

Kama umejifunza basi like share ili na wengine wajifunze pia maswala ya Fedha na mikopo ya benki.
 
Mikopo ina stress sana, kuna mtu kakimbia haonekani tangu mwaka jana mwezi wa 9 kwa sababu ya mikopo.
 
sema uxi wako hautatembea watu wanapenda nyuzi za upuuzi zaidi mfano ngono unatembea kilomita 150 kwa saa
 

My income is X and my expenseses Y, I dont care where the difference comes from,

It is not about knowing wrong from right, but we are facked.
 
Huu uzi una madini. Dawa ya mkopo ni kutokopa. Biblia yenyewe ilishatamka yule anayekopa ni mtumwa wa yule anayemkopesha. Kimsingi unapochukua mkopo moja kwa moja unamtumikia aliyekukopesha kupitia ile hela. Tupambane ya hela yote kuepuka mkopo. Hadi uchukue mkopo basi umeshajiuliza kama mara 976896... saa nyingine biashara inafanya vizuri umeanza kutunza pesa zako benki vinaanza vishawishi. Ndugu KATAA KUKOPA.

Biashara hainaga uhakika 100%. Huwa tunajitahidi kuzingatia kanuni za biashara lakini bado huwezi kuwa guaranteed mambo yaende sawa kama ulivyopanga kwa 100%.
 
Dawa ya mkopo ni kutokopa
Mtoto asisome? Kuna watot wengine hawana mikopo kabisa ya HESLB sasa mtoto asisome? Hakuna anayependa kukopa. Labda sema bond /collateral yakoni ipi? Hapo ndipo kuna shida.
 
Mtoto asisome? Kuna watot wengine hawana mikopo kabisa ya HESLB sasa mtoto asisome? Hakuna anayependa kukopa. Labda sema bond /collateral yakoni ipi? Hapo ndipo kuna shida.
Mbona unanililia kwa matatizo yako? Hata mimi nina yangu. Halafu nimeandika kabla ya kuchukua mkopo uwe umejiuliza sana. Karudie kusoma comment yangu.
 
Kuna jamaa yangu yeye ni loan office bank X, ananihadithia anakuja mteja anakuelezea plan yake kwa nini anataka kukopa huku ana hati ya nyumba, kimoyoni tu anajisemeaga hiyoo nyumba ya kuokota hiyoo. Yaani sema tu ni muadilifu anawakatalia kua hawajakidhi vigezo, vinginevyo ni msiba tu kwa kweli.
Yaani mtu anakopa pesa business plan ni zero kabisa anaulizwa unataka ufanyie nini mkopo anashindwa hata kujieleza.
 
Haswa watumishi wa umma wengi Wana wenge na kufauta mkumbo wanakopa tu kama wanaenda chuo kwamba ni mazeoa kukopa...Wale watu wa bank kutwa wanapiga misele kweny ofisi za umma na kushawishi .

Mwisho wa siku mtu anakopa kwa kufuata mkumbo na ushawishi hajui pia anaenda kufanyia nn.
 
Kuna shida sana kwenye jamii zetu hizi haijalishi amesoma au hajasoma wote wamo kwenye janga hili Mungu tu asimame nao
 
Kiufupi mikopo ni utumwa,hasa hii ya watumishi..ukijiingiza ni vigumu kutoka.ni mwendo wa kutop up tu mpaka unastaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…