Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MOJA YA MAMBO YALIYONIFANYA NICHUKIE AWAMU YA TANO NI SUALA LA UTEKAJI. HATA KAMA WAKOSOAJI NI WAPUMBAVU BASI USITUMIKE UPUMBAVU KUKABILIANA NAO.
Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli
Suleiman aliwahi kusema,
Mhubiri 7:17
[17]Usiwe mwovu kupita kiasi;
Wala usiwe mpumbavu;
Kwani ufe kabla ya wakati wako?
Be not over much wicked, neither be thou foolish: why shouldest thou die before thy time?
Huu ni ushauri bora wa wakati wote kwa Watu wote.
Lugha za kejeli bila staha.
Lugha za matusi pasipo heshima.
Mashambulizi ya kudhalilisha utu badala ya kuhifadhi akiba ya maneno ya hekima.
Hakuna anayependa kutunwa. Hata mtu dhaifu kabisa au mtoto mdogo hukasirika atukanwapo.
Hata Mbwa ukimkejeli anaweza kukuuma.
Katika ngazi ya Familia,
Mke anapotoa matusi kwa Mumewe huweza kupigwa makofi na hata kuumizwa.
Mume anapotukana na kumdhalilisha mke wakati mwingine tusikia kesi za kumwagiwa maji ya moto au mafuta
Watoto wanapoleta shida na kuonyesha utovu wa nidhamu hupewa adhabu.
Hii yote ni katika namna ya kuwekana sawa na kutafuta HESHIMA.
Suala la reactions mtu anapofanyiwa dhihaka, dharau au kudhalilishwa hutofautiana baina ya mtu na mtu.
Wapo wenye Hasira wasio na uvumilivu.
Wapo wapole kama sisi Watibeli ingawaje uvumilivu nao unamipaka.
Wapo wapumbavu
Na wapo wenye hekima.
Ingawaje sheria zipo lakini hiyo haiondoi reactions za Watu hao katika kukabiliana na wale wanaoonyesha kuwadharau na kuwadhalilisha.
Taikon na Watibeli wengine hawapendi utekaji. Hatupendi mtu atekwe, kuteswa na kuuawa.
Tunajua utekaji ni kinyume cha Haki.
Ingawaje tunajua pia wanaotekwa huenda kuna sehemu hawakutenda haki.
Tunajua pia wapo wanaotekwa Wakiwa na Haki.
Yaani hawajatukana mtu. Hawajadhalilisha mtu. Kosa lao ni Haki na kusema Kweli.
Watekaji hujui wanayemteka anahaki au hana. Watekaji hupenda kutafuta kisingizio cha kuhalalisha utekaji wao. Wakikosa visingizio hujiona na hatia
Lakini wakipata kisingizio hata kimoja hujipa Haki na roho zao huwa nyeupe.
Kuna Watu hufikiria kuwa Wanasiasa huteswa na damu za wale wanaowaua au kuwateka na kuwatesa. Elewa, watekaji hupata hatia Pale wakijua kuwa mtu wanayeenda kumteka hana kosa lolote na hata walipojaribu kutafuta kisingizio walikosa.
Elewa hata shetani hujihisi hatia pale anapomfamnyia mtu ubaya mtu asiye na kosa lolote. Hata alipotafuta kisingizio alikosa.
Unapomtukana mtu na kumdhalilisha mtu elewa unavunja sheria.
Kwa mfano, kiongozi fulani ni Fisadi au Jizi hiyo haikupi haki ya kumdhalilisha hasa ukiwa hauna ushahidi. Wote mnakuwa wahalifu.
Na hiyo itakuwa ni vita vya wahalifu ambavyo kikawaida havinaga kanuni wala Haki haizingatiwi.
Namna ya kupambana na Mafisadi kwa haki,
Mosi, kwenda mahakamani.
Pili, kama njia ya kwanza itashindikana basi njia ya pili ni viongozi wa dini kuzungumza kutumia ushawishi wao kuhakikisha mafisadi wanapewa haki yao.
Tatu, ikiwa viongozi wa dini watakuwa pamoja na mafisadi basi hatua ya mwisho ni wananchi kuungana kuwatoa mafisadi na hao viongozi wa dini kimabavu. Hapa itahitaji kujitoa kikamilifu kwa wananchi.
Serikali ipinge na kuondoa Watu wasio na hekima wenye maamuzi ya kipumbavu ya utekaji hasa kwa kesi ndogondogo za kutukanana na kukosoana.
Utekaji ni muhimu kwa Watu wanaounda magenge ya kigaidi.
Lakini kumteka mtu kisa katukana matusi ya nguoni au kudhalilisha kiongozi au mtu sio uungwana. Hiyo ni kesi ambayo inaweza kupitishwa kwa njia ya kawaida.
Hata hivyo hekima hizo hazitatumika ikiwa UPUMBAVU ukiwa kwa kiwango cha juu kwa mpumbavu.
Ukiwa mpumbavu kupita kiasi usitegemee hekima itatumika kukuokoa. Kwa maana kadiri upumbavu unavyozidi ndivyo msaada kutoka kwenye hekima unavyozidi kupungua.
Acha nipumzike sasa.
Ijumaa Kareem
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam