Moja ya mambo yanayoifanya Tanzania iwe nyuma kwenye Teknolojia

Moja ya mambo yanayoifanya Tanzania iwe nyuma kwenye Teknolojia

nodetz

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
7
Reaction score
8
Natanguliza shukulani kwa WanaJF maana mmekua mchango mkubwa sana kwa watanzania wengi kupata maarifa ya mambo mbalimbali hasa kuhusu Teknolojia

Kama title inavyojieleza hapo juu na haya ni maoni yangu kuhusu nchi yangu pendwa Tanzania inavyo litazama jambo hili na jinsi ambavyo inashindwa kupiga hatua katika teknolojia.

Kwanza nianze kwa kukiri kabisa nadhani hata wewe msomaji utakubaliana na Mimi nikisema nchi hii ina vijana wengi wenye vipaji na kujitolea kwenye Teknolojia.

Mfano nimewai kusikia vijana waliofanya vitu vingi tuu vya kushangaza na kuvutia wengi kweli.
na kila mtu anaushuhuda binafsi wa kuthibitisha Hilo iwe ni aliona kwa macho au kusikia redioni au ata mtandaoni, yote kwa yote nikwamba tuko na vijana wengi mungu kawabariki vipaji hivyo.

Lakini kitu ambacho unaweza husielewe ni vipi watu Hawa wenye vipaji wanashindwa kuendelea na kutoa mchango wao katika jamii zetu? Na hatuwaoni tena au kusikia wakifanya vitu vile tulivyo sikia Wana uwezo mkubwa wa kuvifanya.

Ili kujibu swali Hilo kwanza lazima tujue sababu zinazo toa uwezekano wa wao wasifanikiwe.

1. Mamlaka hazitoi ushirikiano kwao.
2. Wanapewa ushirikiano na kuendelezwa lakini wanalewa na vitu wanavyo patiwa kama zawadi na kujikuta wakiliacha lengo lao la kujiendeleza.
3. Hawapati ushirikiano kutoka katika jamii.
4. Hawajiamini na pale wakikutanaa na upinzani hasa kutoka nje basi uacha kufanya
5. Hawana umoja Kati yao.

Zipo sababu nyingi ila hizi nahisi ndizo hasa husababisha tatizo hili
Lakini Leo naomba niongelee moja tuu maana nyingine zimeisha semwa sana hasa ya kwanza kuhusu serikali kutokutoa ushirikiano na kuendeleza vipaji hivi hapa nitakua tofauti kidogo

Nataka niongelee ushirikiano maana naamini huu ndo msingi wa vijana wetu kutambulika na na kutoa mchango katika teknolojia.

Watu wengi uilaumu serikali kwa kusema haijajitoa vya kutosha kuiinua sekta hii ya teknolojia.

ndio japo hili linaukweli kwa kiasi furani lakini naweza kusema Sio kwa asilimia kubwa kwa maana serikali uenda haioni umoja na maendeleo na mwamuko wa vijana wengi na hata jamii kwa ujumla kutumia teknolojia ili kutatua changamoto zilizopo katika jamii zetu.

Ubinafsi ni tatizo ambalo wanalo binadamu wote lakini ubinafsi ulioko katika tasinia ya tehama hapa Tanzania huu ndio mwiba unao ichoma teknolojia ya Tanzania.

Watu binafsi na taasisi zilizoko katika ngazi Fulani au wanao weza kudhibiti kwanamna Fulani maarifa au taarifa kuhusu tehama wamekua wabinafsi sana.

Kwa mfano mtu anaweza kupata wazo la kuanzisha mradi mfano kuunda web application ambayo anataka itoe huduma ya kufundisha watu lugha ya kiswahili (ni mfano tuu)
Asa kwenye mchakato wa kufanya yote haya anaamini kwamba anaweza kufanya yote peke yake bila kushirikisha mtu yeyote na akamaliza.

Sawa hatukatai inawezekana lakini ukweli nikwamba utafanya chini ya kiwango kabisa kiasi ukipeleka hii app yako kushindanisha na za watu wengine utajikuta umefanya kitu ambacho hakina ubora.
Kwa kosa la kujiona unaweza Kila kitu.

Ukweli machungu ambao watu kwenye tasnia hii hawataki kusikia ni ushirikiano na kufundishana namna mpya na Bora za kufanya mambo.

iko hivi jamii ya watu wanao amini katika ubunifu na Teknolojia lazima waungane wawe kitu kimoja na wawe na nguvu moja ambayo hata ikisema jambo ni rahisi kusikilizwa uko serikalini na hawa ndio watakua wanajua changamoto zilizopo na namna ya kuzitatua.

NB: Moja ya aibu kwa taifa nimeoina mwaka huu ni pamoja na yule robot wa bungeni ase ni vituko.

Sijui kilitokea Nini ila Ile ilinifanya nifikilie huenda serikali au wizara inayohusika na tehama hawana taarifa na hawajui kama nchi hii Kuna watu wanaweza kufanya kitu Bora kuriko tulicho kiona pale bungeni.

Na hii ni kwasababu watu wenye uwezo wa kufanya hivyo (vijana) hawana umoja Kila mtu anafanya vitu vingi pekeyake bila kuwa na mwelekeo utasema amekatwa kichwa.

Hitimisho:

Tunaitaji umoja kama tunataka kuisogeza nchi yetu katika ramani ya teknolojia.
Na tuweke ubinafsi pembeni ili twende mbele.

Kama unaamini katika kujenga umoja katika teknolojia basi Niko na mawazo mengi zaidi ya Nini tufanye basi tunaweza kuanza kwa hatua ya kuwaunganisha watu wa tehama

Mawasiliano: 0757914834
 
Back
Top Bottom