Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Moja ya zawadi bora baba unayoweza kutoa kwa watoto au mtoto wako ni uwepo wako, ndio uwepo wako kwa hao watoto ni zawadi, utawapa kujiona kuwa unawathamini na kuwajali kwa kuwa karibu nao, kuzunguza nao, kucheza nao na kuwasikiliza wanasema ninj kwako kuhusu mahitaji yao, na maisha yao kwa ujumla.
Moja ya kitu wababa wengi wananyima watoto wao ni muda wa kuwapa watoto, huishia kutoa mahitaji ya chakula na malazi, ila wanasahau kuwa watoto wanahitaji pia muda wako, uwepo wako ili kuweza kujenga husia njema dhidi ya wewe baba na watoto, watoto wanamambo mengi ambayo wanahitaji kuyasikia na kuyasema kwako pia baba.
Wababa wengi wamekuwa wakisema wana majukumu ambayo ndiyo sababu inayofanya uwepo wao uwe adimu kwa watoto wao, ni kweli lakini fanya kila linalowezekana kutenga muda wa kukaa na watoto wako kuwasikiliza na kujua wanakabiliwa na nini katika maisha yao.
Pia kuwaambia nini unataka kwao na kuwapa maneno ya kuwajenga na kuwaelekeza ikiwemo na kucheza nao ili kutengeneza mahusiano( bond) kati ya baba na mtoto ambayo ndio kumbukumbu ya hisia njema inayobaki moyoni hata wakiwa wakubwa.
Mpe mtoto uwepo wako, mfanye akufurahie, atakumbuka hali hiyo maisha yake yote.
Je, Baba unatoa muda na uwepo wako kwa wanao?