Mola by Ngwair, Jay Mo & Bamboo

Mola by Ngwair, Jay Mo & Bamboo

Lyrics Master

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
479
Reaction score
670
Verse 01: JayMo

Mwenyezi nihurumie kiumbe Chako/
Mbele nitafikaje bila mwelekeo wako/
Kwenye Giza siwezi ona bila mwangaza wako/
Mja wako Niko chini ya miguu yako/
Naomba uninusuru na haya majanga ya dunia/
Maana kila kwenye kumi napata tisa na wanalia/
Nadata, sababu tu sio ya ugumu wa maisha/
Naogopa, magonjwa kibao yanaongezeka/
Malaria yanamaliza tulio kwenye Hali joto/
Kipindupindu nacho chazidi kuua watoto/
Wazee wetu wanasumbuliwa na Kansa na BP/
Je vile vidonge vinavyotibu ukimwi vipi/
Groupies kibao wanataka niwape vitu/
Nani yupo salama na nani mwenye virus/
Niepushe balaa niweze kubaki salama/
Na wale wote wanaoumwa bariki waweze kupona/
Washikaji zangu wengi wamefungwa jela/
Ewe Mungu wangu niweke mbali na misala/
Niwe safe, niwe fresh Yani nisiwe majalala/
Bila wasi me nahisi utasikiliza zangu Sala/

Chorus: Ngwair (RIP)

Leo nakuja kwako Mola naomba unipokee/
Na maovu yote naomba unisamehee/
Na Say oooohhh! oooooh! Naomba unipokee/
Na say ooooh! Oooh!! Naomba nisameheee/

Verse 02: Ngwair (RIP)

Najivunia kuwa mi Leo hii, mwenye bahati ndio nahisi/
Niliyoyafanya mpaka naona kama sistahili kuwa hapa/
Ni mengi niliyokosea,hukunisema hukunichapa/
Ya dunia ukichanganya na ujana/
Starehe nyingi mpaka kumsahau baba na mama/
Maisha ya tamaa, ndoto ni kutajirika/
Hata Bill Gates ulichompa nahisi hajaridhika/
Wengi wanataabika/
Ukimwi,umaskini Je Mungu wao nani!?/
Au wao wamekosa nini!? Kwanini!?/
Ndio maana Sina budi kukushukuru/
Ni mengi umeninusuru/
Naogopa nisije kufuru/
Moyo wangu umejaa hofu/
Naona usiniache njiani mi bado mpofu/
Bado nayawaza maisha yangu baada ya kifo/
Nawaza vipi nitaweza kuiona pepo/
 
Back
Top Bottom