Mollel na Laizer waachiwa huru: Demokrasi ndani ya CCM imebakwa?


Kila kitu kiwekwe wazi...Kuwa UAMUZI WA KWANZA ULIKUWA TAKUKURU, NA PIA UAMUZI WA PILI NI WAO TAKUKURU!

SASA HIZO ASSUMPTIONS ZA KINA LOWASSA ZITAWEKWA WAZI HAPO HAO TAKUKURU WATAKAPOJIELEZA KUWA NI KIVIPI WAGANYIKE KWENYE ISSUE NYETI KAMA HIYO KAMA KWELI WOTE NIA YAO NI MOJA!

NA HAPO TUNARUDI KWENYE FACT KUWA TAKUKURU IS NOT RELIABLE NA MAAMUZI YAO YACHUNGUZWE NA WAITWE BUNGENI KUHOJIWA NA SI KUWAACHIA WAENDELEE KUTOWA KAULI NA MMAMUZI YA KISIASA!
 
Walichofanya TAKUKURU ni kuogopa kibao kuwageukia kwa kumuachia Chenge anendelee kupeta na kashfa yake ya BAE-SFO, kibano kuhusu Richmond na EPA.

Bottom line ni kuwa Serikali kupitia TAKUKURU iliwasha moto ambao haikujua ungegeka mwelekeo na kuanza kuwaandama wao wenyewe Serikali.

Huku ni kulindana kunakofanywa na CCM na Serikali chafu!
 
TUKUKURU imesema kwa nini inaachia kesi? Kwa nini hiki ki habari hakijaandika hilo?
 
Ngoja usikie kiasi ambacho TAKURURU imeshakitumia kwa kuendesha kesi hii hadi hapo walipoamua kubwaga manyanga ndio utajua hela zetu wavuja jasho jinsi zinavyotapanywa kwa sababu za kipumbavu!
 
ccm ni mali ya hao nilio wa bold hapo juu kwani siri ni ipi? si hao hao walioanzisha slogan ya ccm ina wenyewe? si ni hao? kwa nini kuuliza jibu mch?
Wakulima na wafanyakazi walishanyang'anywa chama zamani za kale ila hawafahau tu kwa kuwa "NI SIRI YA SERIKALI"
 

Wakuu muwe mnakumbuka, tuliyasema haya mapema kwenye dataz za kutoka kikao cha cc, ambako Kingunge alitaka hawa wabunge wafukuzwe CCM, lakini akazimwa na muungwana, kwa kuwa ilikuwa clear kuwa aliyehusika kuwashikisha alikuwa mzee wa kuonewa na kamati ya Mwakyembe, kwa sababu hawakuwa watu wake,

na tukasema kuwa kuna wajumbe wa cc waliomtaka muungwana kuifuta hiyo kesi mara moja, kwa sababu iatiletea matatizo makubwa ccm na wamasai, kwa vile ushahidi haukuwepo kabisaa, shillingi laki tatu za bongo haziwezi kununua ujumbe hata wa nyumba kumi na hela zenyewe wala hazikuwa za polisi wala Tukukuru sasa zitakuwaje ushaidi mbele ya sheria?

Sasa naona maoni mengi sana hapa ya kulaumu serikali na ccm, hapana wakuu ukweli ni kwamba kama kuna waliokuwa wanafuatilia hii ishu toka ilipoanza ukweli ulikuwa clear kuwa hakukuwepo na ushahidi, kwa hiyo hata kesi yenyewe haikuwepo toka mwanzo.

Tunafurahia huu ushindi kwa wabunge kwa sababu ni message sent kwa mzee wa Richimonduli kuwa pamoja na yote ya kuihujumu nchi yetu anayoyafanya, bado yuko on the wrong side, ingawa tunajua kwua sasa anasaidiwa na almost viongopzi wote wakubwa, lakini bado tunaamini kuwa kwenye ukweli uongo hujitenga na atashindwa tu na kulegea!
 

Takukuru Inawajibika Kwa Wananchi Kwa Kupitia Bunge Na Si Chama!
 
Takukuru, kuna wanaodhani kuwa ni mali yao, sasa uamuzi wa hii kesi ni clear kuwa mawazo yao yalikuwa mufilisi,

na kwamba Takukuru ni chombo cha wananchi na kikitumiwa vibaya kwa manufaa ya kiongozi flani,

basi mahakama itawasimamia wananchi kama ilivyofanya kwenye hii kesi!
 

Swala kubwa ni kuwa, kama alivyosema Mushi hapo juu, ni lini na vipi TAKUKUKURU itawajibishwa? Personally I think it is a big failure with neither the integrity nor the will power to perform it's task.
 

HII inadhihirika kwa takwimu zisizo rasmi kuwa, wengi waliopo magerezani ( say 90%) ni watu wa kipato duni......!
 


Hakukuwa na kesi tangu mwanzo, huwezi kumkamata Mtanzania na shilingi laki nne na kusema alikuwa anataka kuzitumia kwa ajili ya kuhonga wajumbe wa mkutano, na hapo hapo unawahusisha Wabunge na pesa hizo. Huitaji kuwa criminalogist kugundua kuwa pale kulikuwa na mchezo wa kuhangamizana kisiasa. Suala hapa ni kwa jinsi gani TAKUKURU inaweza kutumika kwa ajili kukomoa watu, nafikiri hili ndilo suala la kujadili.
 

Mushi una haki ya kupinga, lakini naweza kukwambia wazi kuwa TAnzania ukiwa fisadi jela si kwako, au ukiiba pesa nyingi na ukahonga kwa maslahi ya "wenzetu" jela si kwako. Nenda ukaibe kuku uone cha moto.
What i mean is, the war is just begining, it will take time for the criminals to face justice and pay for their crimes, not now. Kuwapeleka mahakamni na geresha tu, makosa walifanya lakini kuwafikisha gerezani kwa makosa yao bado sana. I am sure you know this. Tunachopiga kelele ni walau wezi waache kutuibia, wajue tunajua na wajue kuwa wanajua kuwa wanatuibia. Hii ni kazi ya kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…