Moloko Kibwana Jifunzeni V Pass

Moloko Kibwana Jifunzeni V Pass

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kama watafikishiwa ujumbe kwa njia yeyote basi itakuwa kheri kwetu
Nashangaa benchi la ufundi kwa kipindi kirefu sasa wameshindwa kulisimamia hili

Ni ukweli usiopingika wachezaji wetu Jesus moloko na Kibwana Shomari kwa mara nyingi wamekua wakifanikiwa kuzipenya ngome za wapinzani na kukikaribia kabisa kibendera pembeni huku lakini kosa la wote hao wawili ni kutotulia na kupiga v pass,wanachokifanya wanaupiga ule mpira wakimlenga golikipa!,najiuliza hivi tatizo hili lililodumu kwa misimu karibu miwili hivi mbona halirekebishwi?Mwalimu Nabi na Kaze hamlioni hili mkalipatia ufumbuzi?wachezaji wenyewe husika hivi huwa hamuangalii mipira ya ulaya? Jifunzeni basi kipitia hata hili kombe la dunia muone assist nzuri za V pass ambazo hadi sasa zimepelekea magoli zaidi ya sita yaliyotokana na pass hizo.

Natumai taarifa hii itawafikia kwa njia yeyote na mjirekebishe.Faridi huwa anajitahidi kwa hili,Djuma shaban nae ingawa anatakiwa aongeze juhudi..
Tumeonaechi iliyopita Mayele amepewa assist V pass toka kwa Denis nkane ambayo ilizaa goli zuri.ila Nkane angesema apige kama mnavyopiga nyie tusingepata bao.

Unbeaten iendelee...

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Hili ni tatizo linalowasumbua kwa muda mrefu. Sina hakika km kocha huwa anazungumza nao na kuwaelekeza ili wajirekeboshe au hawawezi kubadilika!
 
Back
Top Bottom