Mombasa Republican Council wanataka nchi yao...


point noted.
Serikali za kiAfrika zimeyataka haya,
mfano ni jinsi mikoa ya kusini ya Tanganyika ilivyokuwa nyuma kimaendeleo pamoja na kuwa na rasilimali zote.
Mfano wa ujinga wa karibuni ni huo mradi wa bomba la gesi kutoka sijui ni Ntwara vile, mpaka Dar es salaam, kwanini power plant isijengwe kule, halafu umeme ukaingizwa mu-gridi ya taifa.
Ujinga tu!
 

umesomeka GT!
 
Kimsingi mipaka aliweka mkoloni, sasa kuna taabu gani na sisi tukiweka yetu ambayo tunadhani itakua na manufaa kwetu?

hili nalo neno.
Moja ya athari za mipaka ya ukoloni ni kuyatenga makabila,
mfano Wamasai katika Kenya na Tanganyika, na Waluo katika Kenya na Uganda, bila kusahau Wasotho katika SA na Lesotho...
Tuweke ya kwetu bwana...
 
Huo ni urithi aliouacha mwarabu ktk pwani yote ya africa mashariki hadi kusini, wakati wakoloni wenzao walikuwa wanajenga makanisa kwa ajili ya kuwafundisha watu kwenda mbele za mungu kwa hofu,shule kwa ajili ya kupata makarani na wasaidizi kwenye utawala wao na mahospitali kwa ajili ya afya za watu wao wa kuwatumikia hao vipofu waliendelea kuwafundisha waswahili kuvaa kanzu ya kutofanya kazi ila biashara zisizo na tija ( zisizolipia ) matokeo yake ndiyo hayo.
 

hiyo elimu tulopewa na hao wazungu imetusaidia nini??
naona bado tunazidi kudidimia kwenye umasikini, bora ya hao waarabu hawafi na njaa
 

maybe.
Lakini usiwe biased, take your time upitie malalamiko yao, then ndio uhitimishe.
 
hiyo elimu tulopewa na hao wazungu imetusaidia nini??
naona bado tunazidi kudidimia kwenye umasikini, bora ya hao waarabu hawafi na njaa

point noted.
 
Mimi hua najiuliza swali moja. kwanini MRC watake kujivuta kando na kutaka nchi yao? Na nikiangalia kwa undani, sipati jibu kamili. maana kama ni kutaka kujikimu kimaendeleo, sioni wakitoboa. Ombi hilo la kutaka kujivuta msingi wake ni wa kidini na sio ya kujali maslahi ya wadigo au wagiriama ambao shida zao za kawa sote tunazielewa. Hivi miaka tatu iliyopita 2008, rais wa Iran amedinajad alizuru mombasa, huenda ikawa mvuto ambao kundi haramu la MRC unao inachochewa na ziara hiyo.
 

wewe ndio ulietia udini kwenye comment yako.
Kumbuka kuwa mkoa wa Pwani hauishii tu ufukweni kwa waswahili, unasogea mpaka miteremko ya Ml. Kilimanjaro sehemu za Voi na Taveta, na kule kaskazini unaenda mpaka Garsen, na kwenye mpaka wa Pwani na North East, jirani kabisa na mji wa Garissa, na wakazi wa huko kote, ambao sio waislamu, wanashiriki harakati hizi.
Huo udini unatoka'pi?
Kwa hiyo we have to trace back tujue ni nani mwenye alitembelea Mombasa recent years? Nadhani Ahmadinejad alikuja kwa ziara ya kirais, na sio kijasusi. Inashangaza kuona unamtuhumu rais wa jamhuri kwa tatizo kama lile, ingekuwa yeye ndio muasisi wa chokochoko hizo wala asingehitaji kuja binafsi, angetuma tu agents.
Sawasawa?
 
kama hiyo ndio hoja kua kwa vile rasilimali nyingi ziko kwao ndio wanendelee kuliko wote mbona hapa tanzania wasukuma ni maskini wakat utajiri wa madini uko kwao tena kwenye ardhi wanayoishi na cjackia msukuma akidai wajitenge ili waendelee! ni small minded people tu hawana lolote!
 

labda pengine walikuwa wameshadai kwanza kutambulika ikashindikana,
who knows?
Viongozi wa Kiafrika hawana muamana ati...
 
Sultani at work, working hard to bring back his Influence over fomer colonies. Lets see mwishowe utakuwaje?
 
Sultani at work, working hard to bring back his Influence over fomer colonies. Lets see mwishowe utakuwaje?

do you reckon that Zanzibar will be that proclaiming Sultan's next step after Indian shores of Kenya?
 
Kikubwa na kizuri zaidi wanadai nchi yao (Pwani ya Kenya including Mombasa) ni sehemu ya Zanzibar....:A S-coffee:

Ina maana wanataka kujiunga na Tanzania. Duh hiyo ndio out of frying into the fire!
 
Wanachogombania ni kile kile ambacho binadamu yeyote mpenda haki anakihitaji.Yawezekana maana halisi ikapotoshwa kwa sababu mbali mbali jazba na upeo wa kujenga na kusimamia hoja.Upole wao na ukarimu wao ndio umewaponza wakamezwa.
 
acha pumba mkuu.
Na serikali yetu inavyotembeza bakuli nayo imeathiriwa na Waarabu?
Na mbona nchi za Kiarabu ndio zenye maendeleo hapa Afrika?
Unaweza linganisha Tanganyika yako na Misri, Libya, Tunisié au Maróc?
Take your time to think berore posting,
anyways, refer the heading above.
 
Wanachogombania ni kile kile ambacho binadamu yeyote mpenda haki anakihitaji.Yawezekana maana halisi ikapotoshwa kwa sababu mbali mbali jazba na upeo wa kujenga na kusimamia hoja.Upole wao na ukarimu wao ndio umewaponza wakamezwa.

wewe umesema la maana.
Kuna watu wanatumia peripherals kukwepa hoja msingi. Kama alivyofanya Pinda v/s Dkt. Ulimboka (MD)...
Unadhani MRC watafanikiwa kwenye move yao? Na nini mchango wa mataifa yenye ushawishi katika kufanikisha azma yao?
 

Mwanzo ngoma ni lele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…