Mondi platinumuz anaelekea kuwa level ya Michael Jackson

Hivi Diamond ameshakuwa na fame kama ile ya:-

Mr. Nice?

Mbilia Bel?

Awilo Longomba?

Kanda Bongoman?

Koffi Olomide?

Fally Ipupa?

Jose Chamileone?

Brenda Fassie?

Usher Raymond?

Akon?


Daaah.....Kama bado, ni kwanini hao hapo juu hawakulinganishwa na Michael Jackson?
 
Nyimbo za bongo flava bhana huwa zina maajabu yake,Utasikia imevunja record huko You tube lakin tuzo zikitokea una shangaa hata kwenye category hazimo,Hapo ndo huwa nashangaa tu.
Wanakua wamepresent pumba
 
Hahaha Huyo Beyonce. .Kuna wakati alijikuta mungu mtu akawa ana mjibu shit Janet Jackson. .Daah nilimshangaa sana
Unaarufu kna kipindi unaweza mfanya mtu akawa kituko ndo kama hivyo.
MJ atabaki level zake,hawa kina beyonce watafatia,tukimalizia kwa platnum nahisi akae kwa kna fally ipupa hvi
 
ila mashabiki wa diamondplatnumz mko na shida sehemu,wote tunafurahi jamaa navyotubeba ila wenzetu mnaharibu.

yupo mmoja akaniambia diamond kwa sasa,hakuna msanii yeyote africa anayemsumbua zaidi ya davido,nikauliza vipi wizkid,akajibu wizkid lofa tu davido ndio sana,nikajua kijana hapa kipa hayupo golini tena.

kosa kwa mashabiki wa diamond,usijaribu kwa namna yeyote kumtaja diamond sehem ya chini,kabla hata hwajasikia unalinganisha na nani,utapata tabu sana.
 
Kwenye hiyo aya yako ya mwisho nadhani wana Ali Kiba ndio mahali pao. Jamaa muziki wake haueleweki anabenwa na Diamond halafu watu wake wana kelele hatari. Usinielewe vibaya mimi ni shabiki Wa nyimbo za kibongo kuanzia miaka ya 2007 na kurudi nyuma. Pia nyimbo za Western za 90's hadi humo kwenye Dilemma, wasn't me, You remind me na kina Ja Rule, 50, Fat Joe na ma hip hop yote ya mbele kuanzia humo 2007 kurudi nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…