Pre GE2025 Mongela: Tunaingia kwenye uchaguzi na uhakika wa ushindi

Pre GE2025 Mongela: Tunaingia kwenye uchaguzi na uhakika wa ushindi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Wakati vyama na wadau wakianza kujiweka mguu sawa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kina uhakika wa kupata ushindi wa kishindo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu (CCM-Bara), John Mongella baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama 2020-2024. Amesema kwa taarifa aliyopokea amejiridhisha CCM kinaingia katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao kwa uhakika wa ushindi wa kishindo.

Akizungumza baada ya kupokea utekelezaji wa Ilani ya CCM mwaka 2020-2024 kutoka Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga, Mongella amesema kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani chama hicho kina uhakika wa ushindi na kwamba waendelee na kasi ya kuleta maendeleo ili kero zote ziishe.

Mongella ambaye yupo kwenye ziara ya siku saba mkoani Shinyanga kama mlezi wa mkoa huo, pia amewataka viongozi wa ngazi ya mkoa na hadi mitaa kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Snapinsta.app_458591473_392402790306882_5714336232005563777_n_1080.jpg
 
Actually, kwa engagements wanazofanya CCM na wananchi nchi nzima pamoja na mipango mikakati ambayo iko tayari, ni dhahiri CCM itashinda kwa kushindo huo wa serikali za mitaa Nov27, 2024 na ule uchaguzi mkuu pia 🐒
 
Kama kawaida Wananchi wameikubali CCM. Kura zote CCM
 
Back
Top Bottom