Mongella ataka umoja na ushirikiano USHETU

Mongella ataka umoja na ushirikiano USHETU

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, ametoa wito kwa wananchi wa Ushetu kuendelea kushikamana na chama hicho ili kuleta maendeleo endelevu katika maeneo yao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Bulungwa, Mongella aliwasihi wanachama na viongozi wa CCM kuwa na moyo wa upendo na mshikamano, hata kwa wale ambao kwa sasa wako upande wa upinzani.

“Hata tunapoenda kutangaza maendeleo, hata tunapoenda kutafuta ushindi wa serikali za mitaa, ndugu zetu hao wengine jamani tuwapende, tushikamane nao. Inawezekana wapo huko lakini kimoyomoyo wanatupenda CCM,” alisema Mongella mbele ya umati wa wananchi, akaongeza kuwa juhudi za chama hicho za kuleta barabara, umeme, maji, na elimu zimeonekana na zinaungwa mkono na wengi.

 
Back
Top Bottom