Kipanga wa hisabati huyo. Aendelezwe. Anyway, unaweza kutusaidia ana umri gani na anasoma darasa la ngapi? Itatusaidia kujua kama kweli ni kipanga au la maana mtoto wa darasa la 1 hadi la pili siku hizi alishajua tarehe, muda, wiki, mwezi na mwaka!!!! Pengine binti Monika ni chekechea wa baby class or middle class, maana pre-unit. Japo pre-unit wengine walishajua days, week, dates and months japo kwa kuimba!!! Mwingine angeweza kuleta any number from 1---9 and mix up with numbers 9----1 ili apate kumi kwani watoto bado wako whole numbers. Fraction bado!!!
Fundisho kwa wazazi. Je unapomtuma mtoto mdogo kufanya jambo fulani je unakuwa na hakika kuwa analifahamu??? Je baba huyo alijua kuwa mwanae ana ufahamu na tarehe?? Au ni wale wazazi ambao kazi la kumpa ufahamu mtoto walishaachia waalimu na dunia??? Si ajabu mtoto Monika alichapwa bakora kama member wetu alivyoshauri hapo juu!!!!! Hapo ni tatizo kama kweli hili jambo lilitokea.