Kadiri ninavyojua mimi, Rose garden ilianzishwa kama bar isiyorasmi pale ilipo, and by then (10yrs ago) it wasnt a big deal at all.
Mwenye bar anajua kabisa yupo pale isivyo halali. Na ndio maana, licha ya kipato kikubwa kinachopatikana ndani ya bar hii, still hakuna uwekezaji mkubwa uliofanywa pale, in terms of infrustructures.
Kama jina lake lisemavyo, Rose garden is only about bar counters, kitchens, hair salons (for men and women) and car wash area, all in a beautiful garden by the road.
Mwenye bar anajua kabisa kuwa yupo pale kimjinimjini tu, sasa kama manispaa ya kinondoni tayari sasa ina plan ya maana ya nini cha kufanya eneo hilo, basi sheria ichukue mkondo wake. But kama manispaa bado haina cha kufanya eneo hilo kwa sasa, basi mwenye bar aachiwe aendelee kufanya biashara.
Bar hiyo ipo hapo for many years, why kalele nyingi sasa hivi, na si wakati ilipokuwa changa. Something is fishy here.....
Mimi sipendi tabia ya maofisa wa serikali kuvunja mali za watu pasi na plan, pasi na sababu ya maana. Wakijidai kufuata sheria ambazo wao wenyewe nao wameshiriki kikamilifu kuzivunja kwa miaka mingi.
Ningependa kuona, wakati wananchi wanaharibiwa mali zao kwa kuvunja sheria, basi na maafisa wa serikali za mitaa/kuu nao wafukuzwe kazi na kufunguliwa mashitaka kwa kutozilinda au kukiuka sheria hizohizo walizovunjwa wanachi. Ndio kabisa, sababu IT TAKES TWO TO TANGLE......
Hauwezi kuniambia kwa miaka 10 ya Rose garden manispaa ilikuwa haoni kama ipo pale kinyume cha sheria.
Ujumbe kwa mwenye bar, kama wenye nchi yao wameona umekwishachuma vya kutosha na sasa inabidi uende zako, basi nawe uondoke utafute eneo lingine la kuwekeza. Haya uliyajua fika kama yatakufika, hata kama kwa kuchelewa.... You should have had Plan B brother.