kisungu
JF-Expert Member
- Feb 20, 2013
- 788
- 266
Hivi hii elimu yetu inaelekea wapi, leo katika kipindi cha watoto cha redioni nikasikia mwendesha kipindi anamuuliza mwanafunzi wa darasa la nne huu ni mwezi wa ngapi kwa kiingereza, mwanafunzi akajibu kwa kujiamini, month six akimaanisha mwezi wa sita yaani June. nimekasirika sana nikafunga redio nikaenda zangu mtaani.