MORAL DILEMMA

AQueen

Member
Joined
Nov 15, 2017
Posts
12
Reaction score
3
Ni mke... uko nyumbani mchana mmoja.. ghafla anaingia mume wako akiwa anatweta jasho na kwa kumuangala vizuri unaona ana damu kwenye nguo na mwilini kiasi.. Anaingia ndani anakusimulia kilichotokea...
Kwamba deal na mshikaji wake halikwenda vizuri.. things got worse.. they fought and he killed him..

A short while after.. akiwa kesha oga na ku change. Polisi wanafika nyumbani kwako wanamchukua kama mtuhumiwa wa kukisiwa..
Kesi inasikilizwa mahakamani.. amekana mashitaka... na amekutaja wewe kuwa shahidi.. (alibi) wake kwamba wakati wa tukio mlikuwa wote nyumbani..
Unaitwa ujibu....[emoji15]
Je unapaswa kutoa ushahidi upi?
 
Ngoja waje wajibu maana umesema kwa wanawake
 
Ngoja waje wajibu maana umesema kwa wanawake
Hata wewe mwanaume waeza jibu... Suppose.... kama ni mkeo ungemtegemea afanye nini.. ? Au kama ni dada yako ndo anakuomba umwambie cha kufanya..... mfano.
 
Unavoenda kuapa mahakamani kwa kutumia biblia au msaafu ukaapa kwa Jina laMUNGU ni bora kukataa ushahidi kuliko kumtetea mtu ambae hujui hata tukio lilivokuwa
 
Kwenye common law jurisdictions nyingi kuna spousal privilege mke/mume akiwa na ushahidi mume/mke wake kavunja sheria anakubaliwa kukataa kutoa ushahidi dhidi ya mume/mke wake.

https://en.wikipedia.org/wiki/Spousal_privilege

Lakini, hilo halijibu swali la, kama mume/mke kakuomba udanganye, utafanyaje?

Mimi jibu langu ni kwamba, njia nzuri kabisa ya kuacha kuvuta sigara ni kutoanza.

Kwa hiyo, maana yake nimejitahidi kuwa na mwanamke ambaye hawezi hata kuua nzi.

Hivyo swali hilo halitakuwepo kwangu.
 
Ushaidi hapo ni kumlinda mmeo,wewe ulitakaje si kuihakikishia mahakama ya kwamba kweli nilikua nae nyumbani siku ya ilo tukio likitokea ukiwa mbunifu zaidi unaleta na uongo kuwa kweli...mahakama ipo kwaajili ya wanaojitetea...the stronger ua liar the more safer you create.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…