Si huwa mnamuita chizi, kichaa, mhuni,n.k, leo imekuwaje tena?
Ila yule jamaa mimi namwelewa sana na hata alipoondoka Simba nikijua Simba imepoteza mtu. Kama mnabisha niambieni kwa wale mawinga waliokuja Simba baada yake nani anamzidi BM3?
Tatizo watu wamekaririshwa maisha (Oooh mhuni, mwendawazimu). Hivi nyie mashabiki wa kizazi cha leo mliwahi kuwaona wendawazimu wenyewe kwenye soka:akina Ian Wright, Eric Cantona, Paul Ince, Paul Gascoigne Gaza, Garrincha, na yule Edmund kichaa wa Brazil aliyeitwa 'The Animal' (aliyewahi kumtwanga makofi Ronaldo De Lima kwenye fainali za World Cup 1998 kwa kuleta utoto uwanjani)? Mnajua kwa nini Edmund aliitwa 'The Animal'? Huyu Morrison anaufikia ukorofi wa hao niliowataja?
Lakini hapa Bongo wamekuwepo pia wachezaji wakorofi waliong'ara na tuliwavumilia kwa maana walikuwa na kitu: Said Mwamba 'Kizota', Hamis Thobias Gaga na 'unywaji gongo uliokithiri', Iddi Pazi, Haruna Moshi 'Boban' aliyemtwanga ngumi Emmanuel Okwi kwa kukosa magoli kizembe, na wengineo kibao. Iweje Morrison tumnyanyase hivyo?