Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mazaya,Tunakutakia maandalizi mema na Mungu akuonhoze ukalifanikishe hilo! Lakini chondechonde kazungumze yaliyo ya Uhuru wetu tu!! Mambo ya dini waachie wengine!!!
Mzee hapa Ndio unaharibu sasa, siyo lazima useme pesa zilikusanywa na Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika kulikuwa na haja gani ya kutaja hivyo wakati unafahamu fika huyo bwana alikuwa mweka Hazina wa TANU? Au siku hizi watu hawaruhusiwi kufanya kazi za dini na jamiiIika...
Kuhusu historia ya safari ya Mwalimu Nyerere UNO February 1955 fedha zilichangwa na wanachama wa TANU.
Mkusanyaji wa fedha hizi alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) Iddi Faiz Mafongo ambae pia alikuwa Mweka Hazina wa TANU.
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza kwa kirefu safari ya UNO ya Julius Nyerere.
Kuhusu ofisi ya African Association ilijengwa kwa kujitolea wanachama kati ya mwaka wa 1929 - 1933 ilipofunguliwa na Gavana Donald Cameron.
Haya pia nimeeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Picha ya ufunguzi wa jengo hilo ipo katika kitabu cha Abdul Sykes na hiyo picha inatoka katika Maktaba ya Picha ya Sykes.
Hafla ya kumuaga Nyerere kwa safari hii ilifanyika kwenye jengo la Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika Stanley Street na New Street.
Mazaya,Mzee hapa Ndio unaharibu sasa, siyo lazima useme pesa zilikusanywa na Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika kulikuwa na haja gani ya kutaja hivyo wakati unafahamu fika huyo bwana alikuwa mweka Hazina wa TANU? Au siku hizi watu hawaruhusiwi kufanya kazi za dini na jamii
Mzee Mohamed SaidMazaya,
Labda nikupe historia ya Iddi Faiz Mafungo.
Yeye ni miongoni mwa watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo.
TANU kwa kutambua kuwa alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya wakamuomba awe pia Mweka Hazina wa TANU.
Kadi yake ya TANU ni no.24 na kadi no. 25 ni ya ndugu yake Iddi Tosiri na hawa wote walikuwa wanachama wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Hawa ni ndugu na Sheik Mohamed Ramia wa Bagamoyo na ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kumjulisha kwake.
Najua unatabika kwa kuwa hukuwa unaijua historia ya TANU sasa unapoisoma historia hii ya uhuru unapata mshtuko na kujiuliza, ''Mbona historia inayosomeshwa shule na vyuoni ni nyingine?''
Makwega...Mzee Mohamed Said
Allah akupe umri mrefu wenye kheri na wewe uzidi kutuelimisha.