Morocco hawajabahatisha, walijiandaa vizuri sana siku ile walipofuzu kombe la dunia

Morocco hawajabahatisha, walijiandaa vizuri sana siku ile walipofuzu kombe la dunia

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Hili ni somo kwa vilabu vyetu vya Simba na Yanga vinavyokwenda kushiriki championship kuwa ukitaka kufanya vzr basi jiandae kimkakati mapema kama walivofanya Morocco.

Morocco walipofuzu tu kombe la dunia, walikaa chini, serikali, vilabu vya soka, shirikisho la soka, wafanyabiashara na wadau mbalimbali, wakaambiana kuwa kombe la dunia is not an easy task, you go and meet with giants like Portugal, England, Brazil, Germany, Spain nk.Hata kama walitolewa hao giants lkn mkakati ilikuwa namna gani tunaweza kupambana nao maana anything can happen.

Wakaanza kusaka wachezaji wenye quality ya kukabiliana na akina Ronaldo, wachezaji hao wazawa walikuwa ulaya, wakatumwa watu kwenda kuwafuata na kuwa convince, wakakubali.

Mkakati mwingine ni ushirikiano, kila mdau atoe sapoti kwa sala na dua.

Wamefika hapo sio kwa kubahatisha, Simba na Yanga nawashauri mnakwenda kwenye championship mnaishia robo tu, kaeni angalieni quality ya wachezaji mliokuwa nayo ni ya kufika nusu au final? Mna benchi nzuri la ufundi au mnategemea jezi nyeusi kushinda?

Huo ni ushauri tu

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Haya bana, sisi huku chama hakitaki uraia pacha utafanyaje sasa mkuu?
 
CCM wameua kila taasisi ,raia hawafikiri tena zaidi ya kuwa chawa ,yaani nchi imewafanya watu wake kuwa wasifikiri nje ya box ,maandalizi yanaanzia kwenye kila taasisi yaani kila mtu anahusika kujenga taifa lake lakini Tanzania ukitoa mawazo mbadala unaambiwa wewe sio mzalendo,wewe ni beberu.

Hatutaweza kujenga nchi Kwa mawazo ya kikundi cha watu 200 ,nchi inajengwa na mawazo ya watanzania wote kifupi ni kuwa huo mpira umeshikwa na CCM kiasi ambacho hawawezi kufikiri zaidi ya hapo walipo,

Angalia hivyo vilabu vyote wachezaji kumi na mbili ni raia wa nchi nyingine utapataje vipaji vipya wakati hizo timu umejaza mikurumbembe ya Kongo na Ivory coast?Je bajeti ya wizara inaruhusu kuwekeza kwenye mpira!so mtoa mada usilinganishe Morocco na Simba au Yanga .
 
Wakaanza kusaka wachezaji wenye quality ya kukabiliana na akina Ronaldo, wachezaji hao wazawa walikuwa ulaya, wakatumwa watu kwenda kuwafuata na kuwa convince, wakakubali.



Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
Nilijua unaandika kitu Cha maana mpaka niliposoma hapa nikaona kumbe unakuja na story za kusadikika.
 
CCM wameua kila taasisi ,raia hawafikiri tena zaidi ya kuwa chawa ,yaani nchi imewafanya watu wake kuwa wasifikiri nje ya box ,maandalizi yanaanzia kwenye kila taasisi yaani kila mtu anahusika kujenga taifa...
Unatuletea fikra zako hapa. Hakuna mkakati wowote wa maana ulioripoti.
 
Back
Top Bottom