BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Vibali hivyo kwa wakulima vinawapa ruhusa kisheria kulima na kuandaa mazazo ya Bangi viwandani na kuuza nje kwa mara ya kwanza. Wakulima kutoka maeneo ya Al-Hoceima, Chefchaouen na Taounate wataruhusiwa kuzalisha na kuuza bangi kwa matumizi ya matibabu na viwandani, kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge mwaka 2021.
Shirika la kitaifa linalodhibiti shughuli za Bangi ambalo lilitoa vibali hivyo limesema wakulima watahimizwa kuongeza uzalishaji halali wa Bangi ili kukidhi hitaji la soko. Morocco kwa muda mrefu ilikuwa moja kati ya nchi wazalishaji wakubwa wa Bangi haramu duniani na ilikuwa ikizalishwa kutoka katika maeneo maskini zaidi ya milimani ya nchi hiyo na kusafirishwa kwenda Ulaya.
Hatua ya serikali ya kuhalalisha uzalishaji wa bangi inalenga kuboresha hali ya wakulima maskini na kuzalisha mapato kwa uchumi.