A
Anonymous
Guest
Naomba nitoe malalamiko kwa Serikali juu ya Barabara ya Kilombero Mkoani Morogoro ambayo mwanzo ilikuwa ya vumbi ila Serikali ya Awamu ya 6 imetutengenezea lami, napongeza kwa hilo.
Barabara hiyo ambayo inajulikana pia Barabara ya Ifakara - Kidatu Wilayani Kilombero pamoja na hivyo, shida ni moja haijawekwa matuta, pia pembezoni mwa barabara kuna Shule, matukio ya ajali yamekuwa mengi sana.
Kila siku iendayo kwa Muumba kutokana na vyombo vya moto ikiwemo magari na Bodaboda kuendeshwa kwa spidi kubwa bila wahusika kujali Watu wanaopita pembeni au kuvuka Barabara.
Ombi letu Wananchi, Serikali ifikirie hilo, tuwekewe matuta kupunguza, tunasikitika kusema kuwa kutokana na ajali tumepoteza Watu wengi tunaowapenda.