KERO Morogoro: Barabara ya Kisaki-Mikese ni mbovu, inasababisha changamoto kwa wanaoitumia

KERO Morogoro: Barabara ya Kisaki-Mikese ni mbovu, inasababisha changamoto kwa wanaoitumia

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya kutokea Mvuha kupitia Kibungo Chini Mission kuja mpaka kutokea eneo la Mikese imekuwa kero kwa kila raia anayeitumia, na ajabu ni kuwa barabara hii imekuwa hivi kwa muda mrefu na hakuna anayejigusa.

Cha ajabu ni kuwa kwa sisi wachimbaji wa mawe kila gari tunachangia Serikali kiasi cha Shilingi 105,000/= ambapo 60,000 ni ushuru wa Halmashauri na 45,000 Wizara ya Madini.

Kwa siku gari za madini zinazotumia Barabara hii ni zaidi ya 50+ Hapo sijaongelea mazao ya kilimo na misitu na wasafiri walipa Kodi wa kawaida.

Ajabu ni kuwa viongozi wengi wanaitumia kwenda Mvuha Wilayani na Bwawa la Nyerere, adha wanaiona lakini kwa kuwa magari yao hayakwami sio shida kwao.

Mwaka jana (2024) mheshimiwa mkuu wa nchi alikuwa na ziara Mkoa wa Morogoro hapo tuliona mashine zikikwangua na mashimo kuziba baada ya hapo hakuna jipya tumerudi kulekule.

Je, hii Barabara ni kwa ajili ya nani na kama sio kipaumbele kwanini kutozana ushuru huku hakuna maendeleo.

Kwa sasa kulala njiani siku mbili au tatu kwa safari ya Kilometa 100 ni kitu cha kawaida sana.

IMG-20250129-WA0001.jpg
 
aisee hatari sana labda tuishawishi serikali ijenge ikulu ndogo huko mvuha pengine TARURA/TANROAD wataona umuhimu wa kuijenga hiyo barabara
 
Back
Top Bottom