Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa zimehitimishwa rasmi hapo jana, Jumanne Novemba 26.2024 huku leo, Jumatano Novemba 27.2024 zoezi linalosubiriwa na wengi ni la upigaji wa kura, ambapo kufuatia sera za mbalimbali vya siasa wananchi wanayo nafasi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka
Hata hivyo, katika zoezi la ufungaji wa kampeni hapo jana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati kimeeleza masikitiko yao kutokana na kile walichodai kuwa Mwenyekiti wake wa wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro Ernest Mkami ameshambuliwa na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Baada ya kupata minong'ono ya taarifa hiyo, usiku wa kuamkia leo, Jumatano Novemba 27.2024 Jambo TV imezungumza kwa njia ya simu na Afisa Habari wa CHADEMA Kanda ya Kati Juma Omary ambaye amedai kuwa mgogoro/ mvutano baina ya pande hizo mbili umetokea kwenye kata ya Magoweko, kijiji cha Kisimani, kitongoji cha Uchagani, jimbo la Gairo
Amedai kuwa kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi iliyokuwa imepangwa ambayo pia ilishirikisha vyama vyote, wasimamizi wa uchaguzi na Jeshi la Polisi ilikuwa inaonesha kuwa Novemba 26.2024 CHADEMA ilipaswa kufunga kampeni zao kwenye kitongoji cha Uchagani, kijiji cha Kisimani, kata ya Magoweko na CCM ilipangwa kufunga kampeni zake kwenye kitongoji cha Ungulodi, kijiji cha Matenkini kwenye kata hiyohiyo ya Magoweko, lakini amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida walishangazwa kuona CCM imefunga vipaza sauti na kufanya maandalizi kwenye eneo linalopaswa kutumiwa na CHADEMA kinyume na taratibu
"Yaani kilichotokea ni kwamba wao hawakuwa na ratiba kwenye kijiji husika, kwa hiyo wakati hawana ratiba sisi ndio tulikuwa na ratiba kwa hiyo wakavamia wakiongozwa na Katibu wao Mwenezi Yohana Senyagwa ndio wakavamia na walikuwa watu kama 20 hivi, wakashusha vyombo, wakapiga watu waliokuwepo pale na kuondoka na Laptop na hiyo Printer" -Juma
Ameendelea kufafanua kuwa, baada ya sintofahamu hiyo kutokea CHADEMA walikwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi, ambapo Polisi waliwaita viongozi wa CCM ambapo amedai kuwa kwa pamoja wakajiridhisha kuwa eneo hilo linalogombaniwa lilipaswa kutumiwa na CHADEMA na sio CCM baada ya kupitia ratiba, hivyo Polisi waliwaamuru CCM kuondoka kwen