Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigella ameamuru daktari katika Kituo cha Afya cha Mikumi (jina tunalo) akamatwe akituhumiwa kusababisha mjamzito ajifungue akiwa kwenye pikipiki ya matairi matatu maarufu kwa jina la bajaj.
Shigella alitoa agizo hilo aliposikiliza kero za wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Mikumi wilayani Kilosa.
Wakati wa mkutano huo, kijana aliyejulikana kwa jina la Abdallah Agustino, mkazi wa Mikumi alidai kuwa, Aprili mwaka huu alimpeleka mkewe, Jenifa Francis katika Kituo cha Afya cha Mikumi ili kujifungua.
Alidai walipofika kituoni hapo, daktari aliyekuwa zamu alimueleza kuwa Jenifa alitakiwa afanyiwe upasuaji na akamtaka ampe Sh 120,000 ili atumie vifaa vyake, badala ya kwenda kununua sehemu nyingine.
Agustino alidai kuwa, alishindwa kutoa kiasi hicho cha fedha na daktari alimweleza achague ama kumpa fedha hizo, au aondoke na mkewe.
Alidai walioondoka sehemu hiyo na wakati wakiwa njiani kwenda katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu Kizito cha Mikumi, mkewe alijifungua wakiwa kwenye bajaji.
Akijibu swali la mkuu wa mkoa huyo juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya daktari huyo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Dk George Kasibante, alisema tayari wamebadili uongozi wa kituo hicho cha afya na kumpa onyo mhusika.
Shigela alisema haridhishwa na hatua zilizochukuliwa dhidi ya daktari huyo ukilinganisha na ukubwa wa kosa alilolifanya kutokana na majibu aliyopewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa.
Aliwaagiza polisi wamkamate daktari huyo na kumuweka rumande na kisha akamwagiza Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Morogoro, Manyama Tungaraza, kufanye uchunguzi kuhusu suala hilo na ikithibitika kuna kosa, achukuliwe hatua za kinidhamu.
Shigella aliwataka watumishi wa umma katika sekta ya afya mkoani humo kuacha kunyanyasa wajawazito.