Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MTAA WA SALUM ABDALLAH WA CUBAN MARIMBA CHA CHA BAND
Morogoro wamemuenzi mwanamuziki maarufu Salum Abdallah Yazidi kwa kumpa mtaa ambao yeye aliiishi katika uhai wake.
Kumbukumbu yangu ya Salum Abdallah naivuta kuanzia mwaka wa 1957 niko Mtaa wa Kiungani na Sikukuu nyumbani kwa mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed.
Umri wangu ulikuwa miaka mitano.
Mama yangu huyu alikuwa na gramaphone ambayo alikuwa akipiga rekodi za Septet Habanero kutoka Cuba na rekodi za Salum Abdallah.
Nakumbuka baadhi ya nyimbo hizi mashairi yake na sijui majina ya nyimbo hizi kwa kuwa nilikuwa nikiziimba tu na nilikuwa sijui kusoma.
Nakumbuka nyimbo moja ilkikuwa na mashairi haya:
''...niko chini ya mkungu
Naomba litoke jua niuone ulimwengu...''
Salum Abdallah alikuwa akirekodi na kampuni iliyoitwa Mzuri kutoka Nairobi, Kenya.
Nakumbuka miaka hii kwani wakati mimi nikiimba nyimbo za Salum Abdallah dada yangu mkubwa ambae alikuwa akisoma Girl School yeye akiimba nyimbo ya Everly Brothers, ''Devoted to You.''
Lakini kubwa ni kuwa nilipopata umri wa kujua mambo ndipo nilipofahamu kuwa Salum Abdallah alikuwa rafiki ya baba yangu.
Nimepata hapa kuandika kuhusu Salum Abdallah na siku nilipomuona kwa macho yangu Mtaa wa Stanley na Nyamwezi na huku Swahili ambako kulikuwa na Cuban Marimba Branch.
Nilikuwa napita nje nikaona watu wawili wamekaa mmoja anapiga guitar.
Katika hawa wawili mmoja alikuwa Salum Abdallah.
Baada ya siku hii haukupita muda mrefu Salum Abdallah akafa kutokana na ajali ya gari.
Ilikuwa mwaka wa 1965.
Wakati wa umauti wake nyimbo yake iliyokuwa maarufu ilikuwa, ''Nalia Nasikitika.''

Picha: Salum Abdallah ni huyo wa katikati na kushoto ni Juma Kilaza.