Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Nimesikia tetesi kutoka kwa rafiki wa karibu kuwa serikali inakusudia kujenga kituo kingine cha polisi kwa kushirikisha nguvu za wananchi katika Kata ya Kihonda, ni jambo jema na zuri, binafsi ningeshauri kituo hicho kijengwe karibu na stesheni ya mwendokasi badala ya kwenda kulijenga eneo la youth mission ambako ni mbali na miundombinu muhimu kama barabara na reli:
- Kituo kikijengwa karibu na stesheni ya mwendokasi kitasaidia kurahisisha huduma kwa wasafiri watakaokutana na changamoto za kiusalama wawapo kwenye mchakato wa kusafiri na mwendokasi au mabasi ya kawaida, hapa nazungumzia wasafiri watokao maeneo mbalimbali kuja kupanda treni hiyo pamoja na wale washukao kutoka kwenye treni hiyo
- Kituo kitasaidia wasafiri watumiao barabara ya Morogoro - Dodoma kwa urahisi endapo kituo hicho kitajengwa karibu na highway hiyo badala ya huko pembezoni ambako ni takribani kilomita moja na zaidi kutoka highway na kilomita mbili toka kituo cha SGR
- Kwa kujenga kituo hicho karibu na SGR itarahisisha kukifikia kituo kwakuwa tuta la SGR limeigawa Kihonda katika vipande viwili na sehemu yenye urahisi wa kufikiwa na wananchi wa pande zote ni eneo la karibu na stesheni ya SGR.
- Kujenga kituo hicho youth mission kutaigharimu serikali kujenga barabara mpya ya lami kurahisisha ufikaji kwa haraka na hasa ukizingatia kuwa polisi wanahitaji barabara za uhakika ili kuwahi matukio ya kihalifu